
Bafana Bafana
Na Boniface Wambura
Timu ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ inatarajia kuwasili nchini Mei 12 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania
‘Taifa Stars’ itakayofanyika Mei 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Nyota wote wa kikosi cha kwanza cha Bafana Bafana kinachofundishwa na Pitso
Mosimane wanatarajiwa kuwepo kwenye mechi hiyo, isipokuwa kiungo Steven Pienaar
anayechezea timu ya Tottenham Hotspurs inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.
Bafana Bafana na Stars zote zina mechi ngumu ugenini za mchujo kusaka tiketi za
fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani Equatorial
Guinea na Gabon. Stars itacheza Juni 4 mwaka huu jijini Bangui dhidi ya Jamhuri
ya Afrika ya Kati wakati Bafana Bafana itakuwa jijini Cairo, Juni 3 dhidi ya
wenyeji Misri.
Stars itaingia kambini Mei 7 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo. Wachezaji
Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya, Henry Joseph (Kongsvinger IL,
Norway), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam),
Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF,
Sweden) wameshaombewa ruhusa katika klabu zao ili wajiunge na Stars kwa ajili ya
mechi hiyo.
Kwa habari zaidi za TFF


Habari nzuri hizi mkuu
ReplyDeleteKi2 ha muhimu hapo stars ni kuwa na mazoea ya kushinda hizi mechi na timu kubwa hata kama ni za kirafiki au hata kama hazipo kwenye kalenda ya FIFA..hao Sauzi wasingeweza kukubali kucheza na sisi lakini wameangalia matokeo kwenye kundi letu gumu lenye timu za kiarabu Algeria,Morocco na C.Africa na tupo nafasi ya pili juu ya Morocco na Algeria.Kama haushindi mechi ukialika timu kubwa hazikubali!!.waje nyota wao,wasije nyie tafuteni ushindi..baada ya mechi dunia inauliza matokeo kati ya Tanzania na A.kusini,haiulizi mlicheza na akina nani.Nchi hizi za Afrika magharibi na kati,wana tabia ya kukamiana kwenye mechi viwe vilabu au ziwe timu za Taifa...Africa ya Kati sasa hivi wameshaweka mikakati kwamba wasifungwe mara mbili na Tanzania...Take Care.Uwanja wao wa Barthelemy Boganda(kama mtachezea hapo) ni wa wazi kama kirumba(watu 20000 hivi),'playing surface' siyo nzuri sana..Mungu ibariki TZ
ReplyDeleteWaleteni tu wakinyoe "Kichwa cha Mwendawazimu"
ReplyDeleteWABONGO TUJIPANGE, SI MNAJUA SASA HIVI MICHEZO NI DILI,
ReplyDeleteMOHAMED KINYUNYU