 |
| Mh Naibu Balozi akiwa na wadau wa Reading wakati wa Carnival hiyo. |
URBAN PULSE CREATIVE inawaletea picha za matukio ya Reading Carnival iliyofanyika jumatatu 30.5.11 ambayo ilikuwa ni siku ya Bank Holiday. Kwa mara ya kwanza TA Reading ikishirikiana na TANZ UK waliandaa banda la kitanzania kwa kupika chakula cha Kitanzania na kuuza kwa wadau mbalimbali waliojitokeza kutembelea banda la TA ikiwa ni mojawapo ya mradi wa kuchangia mfuko wa TA Reading. Mgeni rasmi alikuwa Mh Naibu Balozi wa Tanzania Uingereza Chabaka Kilumanga alieambatana na Afisa wa Ubalozini Amosi Msanjila. Kwa ujumla banda ka kitanzania lilitia fora kuliko mabanda yote mengine ya mataifa mbalimbali
Watu kibao toka mataifa mbalimbali walihudhuria
Watasha waliienda misosi ya Kibongo
Msanii wa Zenji Fleva Berry Black (nyekundu)
akiwa na wadau wa Reading
Mdau Frank Eyembe wa Urban Pulse na Berry Black
Nyama choma ilikuwa kivutio kikubwa kwenye banda la Tanzania
Naibu Balozi Mh. Kilumanga akijiandaa kupakua ugali wa mhogo kwa mlenda
Afisa ubalozi Amos Msanjila (kulia) akifurahi na mdau
 |
| Makuku ya kumwaga yakiandaliwa na Ankal Dello |
 |
Timu ya urban pulse ndani ya banda la TA Reading
|
|
Mdau Paul Onyango Kutoka Bongo Fleva (kushoto) akiwa na wadau wa Reading |
Wengi tulikubali TanzUK(Reading) kwa maandalizi mazuri na kuandika meza kwa lishe nzuri za kienyeji(TZ)siku hii ya Reading Carnival 2011.
ReplyDeleteSasa tunaomba mtuongoze vizuri na kwa kasi zaidi ili vyakula hivi tuviagize toka Tanzania kwa wingi ili mkulima mtanzania nae anufaike kama sisi.
Yooote yanawezeka tukikaza mkanda na kupunguza uhafidhina usio wa lazima ktk taasisi husika ktk uchumi(wa soko,mpango na ushindani) wa sasa.
Kwa Ari, Nguvu na Kasi hii tuanze mapema maandalizi ya sherehe za kumbukumbu ya Miaka 50 ya kumng'oa Mkoloni.
MAINA A. OWINO
UK.