Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB,Dr. Charles Kimei
Benjamin Sawe,Maelezo Dar es Salaam

Waziri Mkuu,Mheshimiwa Mizengo Pinda amemteua Bwana Charles Kimei ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa.

Aidha Waziri Mkuu amemteua Bwana Juma Iddi ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.

Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi hiyo ni pamoja na Mh.Didas Masaburi ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAAT) na Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Bwana George Lubeleje ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Mpwapwa.

Wajumbe wengine ni Bwana Severine Kahitwa ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Bwana Mohamed Mkupete ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Bibi Magreth Nyalile ambaye ni Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha.

Pia katika uteuzi huo wapo Mhe.Theresia Msuya ambaye ni Mweneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na Mhe.Amir Nondo ambaye ni Meya wa Manispaa ya Morogoro

Uteuzi huo umefanyika kwa Mamlaka aliyopewa Waziri Mkuu chini ya kifungu cha 57(1)-(3) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa sura ya 290 na ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 16/4/2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...