swiming puli maarufu jijini Dar inapatikana mtaa wa Upanga kati jengo la YMCA na  ABC Bank Corp kuelekea CITI Bank na Peugeot House. Hapa unaogelea bila malipo kwani wakazi wa eneo hilo wana mwaka sasa hawajadhurika licha ya kwamba puli hili lenye umri wa takriban mwaka sasa limechanganyika maji ya mvua na ya kinyesi toka nyumba jirani. Mbele kule kwenye magari pana kiplefti ambacho nacho kinaleta raha hasa utapopita mbio na gari lako. Hongera kwa wazee wa jiji kwa zawadi hii ambayo bila shaka itadumu kwa mwaka mwingine na kuongeza pafyumu inayotoka hapo, pamoja na maji yenye kurembwa na rangi ya kijani kutokana na umri wake
 Ili kukitambua kiplefti umewekewa matairi ili usije vunja sheria ya usalama barabarani
Kwa kuwa ni swiming puli ya heshima na yenye hadhi huruhusiwi kupita kwa mwendo wa kasi...Bila shaka baada ya warsha, kongamano, semina, vikao na mikutano ya wazee wa jiji kufanywa kwa mara ya ngapi sijui, huenda tukawekewa mabenchi na miamvuli ili tustarehe zaidi - Nani kasema Bongo siyo tambarare??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...