Polisi wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tosamaganga eneo la Kitwiru nje kidogo na Manispaa ya Iringa hapo ilikuwa ni kabla ya kuanza kupiga na kurusha mabomu ya machozi.
Wanafunzi wa Sekondari ya Tosamaganga wakikimbia moshi ya mabomu yaliyokuwa yakipigwa na polisi
Mwandishi wa habari wa radio Ebony Fm akikimbia moshi ya mabomu ambayo yalikuwa yakipigwa na askari hao kutawanya wanafunzi hivi punde
Hapa wakikimbia porini kunusuru afya zao

Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivi sasa, wanafunzi zaidi ya 1000 wapo porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.

Hadi hivi sasa mabomu zaidi ya 10 ya machozi yamepigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanadaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu hayo huku wananchi wa Mseke wakikimbia nyumba zao .

Polisi wamewazuia waandishi wa habari akiwemo Mwanalibeneke Mpiganaji wa Globu ya www.francisgodwin.blogspot.com pamoja na Globu ya Jamii ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo.

Hadi hivi sasa hali si shwali katika eneo hilo na wapiganaji waliopo katika eneo hilo wanaugulia macho kutokana na moshi wa mabomu yaliyokuwa yakitumika kuzuia maandamano ya wanafunzi hao wa Shule ya Sekondari ya Tosamaganga,Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Rabbi tunusuru..kwani vijana wa sasa elimu kwao ni secondary, kilicho primary ni vurugu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2011

    SIJUI NIANDIKE NINI MAANA KILA NINACHO ANDIKA NAKIFUTA,SIWEZI KUELEZEA UCHUNGU NILIO NAO.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2011

    jamani? nyie akina ras makunja vipi? sasa hii si noma tupu?mbona nyie mnapendelewa viwalo vipya na maslahi mengine,wanafunzi pia wanahitaji

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2011

    JAMANI SIJUII HATA NISEME NINI HIVI JAMANIHII NCHI INAELEKEA WAPI YAANI KITU IMEKUWA HOVYO HOVYO UTAFIKIRI HII NCHI HAINA VIONGOZI KABISA HAKUNA MWENYE SAUTI UTAFIKIRI NYUMBA AMBAYO WAZAZI WAMEONDOKA WAKAACHA WATOTO WENYEWE WANAVURUGANA YAANI SIJUII HATA CHA KUSEMA JAMA VYAMA VYA UPINZANI WAOMBE MSAADA KUTOKA NJE WAJE WANUSURU NCHI NA WATU WAKE MAANA TZ SIYO ILE NCHI YA AMANI TENA AFADHALI HATA NCHI ZILIZO NA VITA IKAJULIKA MOJA KULIKO HII VITA BARIDI AMBAYO UKIENDA UBALOZINI KUOMBA VIZA KUKIMBIA NCHI YAKO HUPEWI KWA SABABU WANAJUA NCHI INAAMANI LAKINI INGEKUWA VITA INAYOJULIKANA UKIENDA UBALOZI UNAPEWA VISA TZ IMEOZA YAANI HUTAKI HATA KUISIKIA LAITI NINGEKUWA NA UWEZO WAKUHAMISHA FAMILIA YANGU NJE INGEKUWA BORA SANA JK NCHI IMEKUSHINDA KABISAAAA HAKUNA MJADALA MUNGU INUSURU TZ INAYOANGAMIA

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2011

    wajamani watanzania watakimbilia wapi? hajali zizizoisha,maaskari wanauwa raia, wanafunzi maandamano wakidai haki zao za msingi wanapigwa mabomu, hali ya maisha ningumu vitu vinapanda bei kila leo ajira hamna, rushwa imeota mizizi tofauti kubwa ya walionacho na wasionacho.watanzani woote wasali sana na muomba mungu ainusuri hii nchi ya Tanzania inayoangamia hakunamsaa kwa viongozi

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2011

    Tunaambiwa tuombe haki kwa amani. Lakini watoa haki hawako tayari kutoa haki si tu bila kudaiwa bali kudiwa kwa maandamano na migomo.

    Hivi hiyo kauli ya amani itasikika lini ikiwa polisi ndo ngome ya kuzuia haki kwa kisingizio cha amani?

    Hivi amani tuliyonayo haitoshi kwa kila mtu kudai na kupewa haki yake?

    kwa nini mpaka mtu adai haki?


    Mtume alisema "umasikini ni nusu ya uovu" kwa wanaofahamu hadithi hii wanajua neno uovu limetumika vipi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2011

    hivi Tanzania kuandamana hairuhusiwi, kwa sababu kila nnapooana picha za maandamano polis wako pembeni kuyapinga maandamano na mabom juu, so raia hawana haki kuandamana kwa njia yoyote ile. mi nauliza tu naomba msinijie juu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2011

    jamani yanataka yajitokeze kama kipindi kile enzi za dudu mzee mpogole miaka kama 18 iliyopita kupinga utawala wake waliokuwepo nadhani hawa watu ni wasomi serikali ingewasikiliza hawa wasomi
    .........
    mahimbi

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2011

    violance has been and will always be the means to settle our problems. Why? cant fight violance withou violance.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 31, 2011

    poleni sana wadogo zangu mpaka hapo mmeshinda na mmeitangaza shule yenu vile hata huku Ulaya tumewaona. Nawashari mrudie tena mkirudia msiende kwa mkuu wa mkoa, nendeni kwa waziri wa elimu. The other thing maaskari wa watanzania ni waoga,wachokozi na hawajasoma ndo maana si creative, hawana plan wapowapo tu.Cku nyingine msiandamane mkubaliane mkutane hapo kwa mkuu wa mkoa kabla waalimu na maaskari hawajaamka na hawajawashtukia. All da best,nimewapenda sana mmeonyesha umoja na ushujaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...