
Mashabiki damu wa timu ya Chelsea wakiwa katika picha ya pamoja na kombe lao mara baada ya kuibuka vinara wa Fiesta Soka Bonanza mjini Dodoma leo.Ama kwa hakika hili ni tamasha la tatu la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta soka bonanza kufanyika,tamasha la kwanza lilifanyika katika viwanja vya Lidaz Club jijini Dar,tamasha la pili ndani ya jiji la Mwanza kwenye uwanja wa CCM-Kirumba,ambako sehemu zote hizo mbili za awali timu ya mashabiki wa Real Madrida waliibuka washindi, na sasa ndani ya Dodoma ambapo Chelsea wameibuka mabingwa wa tamasha hili na kujinyakulia kombe.

Mashabiki wa timu ya Chelsea wakiwa na kombe lao kwa pamoja jioni ya leo mara baada ya kuibuka vinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti soka bonanza mjini Dodoma leo.



Nasikia kichefuchefu kuona habari kama hii
ReplyDelete