
Kundi la Morogoro Youth Universe of Talents, (MYUT) likiwa limekabidhiwa kreti ya bia ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya zawadi yao kwa kufanya vyema katika shindano la kulisaka kundi kinara la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011,ambalo limefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Four Stars,Morogoro.

Kundi la Morogoro Youth Universe of Talents, (MYUT),likishangilia kwa kishindo huku kila mmoja akimbeba mwenzake kwa furaha kubwa,mara baada ya kuibuka washindi wa shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011,shindano hilo limefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Four Stars,ndani ya Morogoro.Kufuatia ushindi wa kundi hilo,linapata nafasi ya kipekee ya kwenda jijini Dar kwa ajili ya kuchuana na makundi mengine kutoka mikoa mingine ambako mashindano haya yalikwishafanyika,hiyo itakuwa ni kuukamilisha msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta 2011,litakalofanyika jijini Dar hapo baadaye.

Meneja matukio wa kanda ya Kusini wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Albert Nsanzugwanko akilikabidhi kundi liitwalo Gentlemen fulana za Serengti kwa kila mmoja,ambalo lilifanikiwa kufanya vyema na kushika nafasi ya pili katika mchakato wa kulisaka kundi kinara la msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti dansi la fiesta 2011,ndani ya Mkoa wa Morogoro.

Majaji wa shindano la Msimu wa Dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta 2011 wakiwa bize kuandika max za kila kundi lilopanda jukwaani jioni ya leo,kutoka kulia ni Hamis Mandi a.k.a B Dozen kutoka Clouds FM,Msami kutoka THT,pamoja na Kwisa Thomson.

Kikundi cha Cabo Red kikionesha umahiri wake wa kucheza staili ya Michael Jakson kupitia wimbo wake wa Thriller jioni ya leo, wakati wa shindano la kumsaka kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta ndani ya mkoa wa Morogoro,ama kwa hakika ushindani na ubunifu ulikuwa mkubwa kwa makundi yote yaliyoshiriki.

Kundi pekee ambalo pia liliwashirikisaha akina dada wawili,liitwalo Morogoro Youth Universe of Talents, (MYUT) likiwajibika vilivyo stejini kwa namna ya kipekee kabisa,hali iliyopelekea ukumbi ulipukwe na mayowe na miluzi kila wakati,kutokana kundi hilo kuonesha umahiri mkubwa wa kucheza,kwenye shindano la kumsaka kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011 ndani ya Mji kasoro bahari a.k.a Morogoro.

Kikundi cha Moro Skwadi kikionyesha manjonjo yake ya kusakata dansi mbele ya mashabiki (hawapo pichani),jioni ya leo kwenye ukumbi wa maraha wa For Star,wakati wa kumsaka kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011.

Kikundi cha Cabo Red kikionesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma jioni ya leo wakati wa shindano la kumsaka kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta ndani ya mkoa wa Morogoro,ama kwa hakika ushindani na ubunifu ulikuwa mkubwa kwa makundi yote yaliyoshiriki.

Kundi la Gentlemen likiwa stejini likirusha karata yake jioni ya leo katika ukumbi wa For Star,katika lile shindano la kumsaka mkali wa msimu wa Dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta ndani ya mkoa wa Morogoro.

Mmoja wa waendeshaji wa shindano la Serengeti dansi la fiesta 2011,Babuu wa kitaa ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds TV,akisoma makundi yatakayochuana leo jioni,katika suala zima la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011,ndani ya mji wa Morogoro. Picha na Michuzi jr.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...