Taswira ya ujenzi wa Dar es salaam Convetion Centre unaoendelea jirani na chuo cha IFM jijini Dar unaojengwa kwa msaada wa China kushirikiana na serikali ya Jamhuri wa Muungano ya Tanzania. Utapokamilika ukumbi huu mkubwa na wa kisasa utakuwa kitovu cha mikutano ya kitaifa na kimataifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2011

    Miaka kama minne iliyopita niliposoma gazeti kuwa ukumbi huo utajengwa katikati ya mji nilisikitika sana.Pamoja na kelele za foleni barabarani na nyimbo za viongozi wa serikali kuanzisha miji ya pembezoni lakini bado mambo mengi yanapelekwa katikati ya mji.
    Tatizo la foleni na parking halitakwisha kama tutakuwa tunafanya mambo kwa stahili hii.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2011

    Hongera mdau hapo juu kwa kuangalia vitu katika mtazamo chanya wenye kuangalia changamato zinatukabili kabla ya kufanya kitu, hii inanikumbusha shuleni tulipokuwa tunafundishwa unapoanzisha investment yoyote lazima uangalie vitu vingine ambavyo vimezunguuka hiyo investment yako ambavyo vinaweza kuwa changamoto na kuvijengea majibu kabla badala ya kukurupuka kuangalia tatizo la kukosekana kwa ukumbi kama ndo entry point ya kuanzisha investment

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2011

    Mchina anamwaga fweza Africa. Wazungu huku wanakuna vichwa... Kumbe na Kenya wamejengewa uwanja wa mpira kama wetu, nasikia hata nchi za latin America nao pia wamejengewa maviwanja na mabarabara. Western power kwishney. By 2016 China's economy will be similar to US if it continues with the same growth rate.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2011

    Kuondoa foleni barabarani ni kutumia njia mbadala za usafiri. Nahisi sasa wakati umefika Dar es Salaam kuwa na "metro". Kurudisha mabasi ya "Icarus". Kuweka kodi ya magari yanayoingia kuanzia Kariakoo mpaka Posta. Kuweka njia maalum kwa madaladala. Kuiga ujenzi wa barabara za UK. Walichofanya London ni kuwa wamejenga barabara mbili ambazo zinazunguka London, "Circula Road". Hizi huondoa magari mengi ambayo si lazima yapite barabara moja tu kufika yanakokwenda. Ukikaa hapo Morogoro road utakuta shangingi lina watu wawili, dereva na bosi kubwa! Pengine mtu huyu huyo mama watoto naye anashangingi lake na dereva wake, mtu huyo huyo anagari maalum ya watoto, tena cha ajabu wote wanakwenda kazini na skuli hapo Posta. Wenzetu hawa wazungu wanatumia sana taalum katika kufanya mambo yao. Wakati umefika kuwa na "Transport Strategy" kwa kila mji Tanzania.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2011

    vip huo ukumbi utakuwa na uwezo wa watu wangapi?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 14, 2011

    hakukuwa na haja ya kujenga ukumbi huu mpya dar es salaam. jamani Dodoma itahamiwa kweli? tutauimarisha vipi mji ule? kwani kila kitu ni Dar? serikali inatia kinyaa hii!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 14, 2011

    Hili ni lile jengo lililoko jirani na Ocean Road au vipi? Halafu pale ile barabara ya kiungo imefungwa kupisha ujenzi huu.

    Hivi pale parking itapatikana kweli? Na hii Dar es Salaam viwanja vimekwisha maeneo ya Goba na Bunju hata wakajenga pale mjini?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 14, 2011

    Gari zitapark Ikulu??? kama fikra ni kuwa na ukumbi mkubwa kiasi hicho tunategemea kuwepo parking ya kutosheleza gari zaidi ya 500, je hili limezingatiwa?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 14, 2011

    Mdau wa kwanza hata mie nilifungua hii page nikitaka kuandika maoni kama ulivyoandika. Naona kumbe tunaoliona tatizo tupo wengi. Kwanza kunahaja ya kuwa na mji wa zamani, sasa taswira ya Dar ya zamani yote inaisha kwa watu kupenda kujenga katikati ya mji, msongamano ni jambo lingine pia. Jengo kama hilo lisingepaswa kujengwa hapo sasa. Maeneo yapo kama NIC walipowaza kujenga ubungo plaza, Tanesco kujenga ubungo pia. inatakiwa majengo yajengwe nje ya centre ili Dar ipanuke msongmano upungue. Serikali inapaswa swala hili iliwekee nguvu. Mfano kununua kuwanja city centre ungeweza kupata nyumba ngapi maeneo kama Kinondoni, Magomeni unapata space ya kutosha kufanya ujenzi wa kisasa na kujinafasi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 14, 2011

    serikali ieleze wawekezaji Dar si city centre tu. Angali Kariakoo majengo marefu yanajengwa lakini hawaweki park za magari. Ivi hii mipango miji inakuwaje. Je kabla ya kujenga ramani zinakaguliwa na wataalam na kupewa ushauri? Tuangalie tuvyojenga mji wetu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 14, 2011

    FOLENI NI ATHARI TOKEZI ZA UCHUMI WA WATU BINAFSI NA TAIFA KWA UJUMLA.JIBU LA FOLENI KUPELEKA BAADHI YA HUDUMA MUHIMU MAENEO YA PEMBEZONI MWA JIJI NA KUBUNI USAFIRI WA UMMA WENYE HADHI YA JIJI LA KIMATAIFA ILI WATU WAACHE KUTUMIA MAGARI YAO BINAFSI KUJA KATIKATI YA JIJI BILA SHUGHULI MUHIMU.UJENZI WA BARABARA ZA PEMBEZONI MWA JIJI NI MSAADA MUHIMU SANA BILA KUSAHAU USAFIRI WA RELI NA BOTI.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2011

    Hata hivyo, nadhani bado nchi yetu inakosa vipaumbele na mipango makini. pamoja na kuwa ni jambo jema kuwa na ukumbi mkubwa jiji Dar, lakini hii itakuwa na athari kubwa kwa Arusha. Ningekuwa ni mimi ningeuendeleza mji wa arusha kuwa ni wa utalii, mikutano ya kimataifa si wanauita the Geneva of Africa! then ilitakiwa kuusapoti kwa kila hali, mji wa office za kimataifa nk nk. Sasa kuuanzishia ushindani hapo nashindwa kuelewa kabisa. Nawasilisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...