Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Serikali alipowasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akirejea toka Uturuki.
Rais wa Zanzibar na Mwenyakiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea ziarani Uturuki.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Waandishi wa Wahabari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanibar alipowasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.akielezea mafanikio ya Ziara yake.
Mwandishi mkongwe wa habari wa ITV Redio One Farouk Karim akimuuliza swali Rais wa Zanzibar alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, baada ya kumaliza mazungumzo na Waandishi wa habari uwanja wa Ndege wa Zanzibar. Picha na mdao Othman Maulid wa Ikulu Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2011

    Kwi kwi kichwa cha habari

    ReplyDelete
  2. Mikausho MikaliMay 04, 2011

    Mjomba badili basi hiyo heading.Shein anatoka Zanzibar anapokelewa wapi sasa-Mchambawima ?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2011

    Bado najiuliza, hizi protocols za 1947 zitaisha lini? Ujio wa Raisi au kiongozi yoyote yule nchini kwakwe kunasababisha "maendeleo" yasitishwe kwani, watu/viongozi wameondoka ofisini kwenda kumkaribisha mheshimiwa. Jamani, what value does this add to the nation? napendekeza kuwa kama kuna haja ya kujua habari za huko alikotoka kutembea/kikazi, basi, press conference tu inatosha, iwe hapo airport au ikulu punde mheshimiwa akisha pata kupumzika. foleni hazitoisha kwa mwendo huu, maendeleo yatabaki hadisi tu, kila unapoenda ofisi fulani, unaambiwa hakuna wa kukuhudumia, wote wameenda airport.... tubadirike, na viongozi wetu ndio waseme, jamani imetosha!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2011

    Swadakta msemaji hapo juu!
    Hizi protokali ni gharama kwa watanzania. Hakuna haja na bahati nzuri hawa ni viongozi tuliowachagua siyo masultani. Kwa nini tuwapokee! nini mantiki yake na ni kweli muda huo mfupi mambo yote yanaweza kujadiliwa hapo airport?
    Tujiangalie ili tujipange upya.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2011

    mdau wa saa 03.02 umenikuna haswa nikweli ndugu yangu maneno yako haswa yana maana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...