Rais wa zanzibar, Dk. Ally Mohamed Shein na mkewe Mama Mwamamwema Shein wakipata maelezo kutoka kwa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Sendar Gurbuz,wakati Rais Shein akiyatembelea maeneo ya kihistoria ya mjini istambul leo.
Rais wa zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akitia nsaini kitabu cha wageni alipotembelea sehemu ya historia mjini istambul.
Rais wa Zanzibar, Dk.Ally Mohamed Shein na mkewe Mama Mwamamwema Shein wakipata maelezo kutoka kwa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Sendar Gurbuz,wakati akiwatembeza maeneo ya kihistoria ya mjini istambul leo.
Akiwa katika Msikiti ambao sasa ni kivutio kikubwa kwa watalii mjini istambul,nchini uturuki.
Hili ni jengo la kihistoria katika mji wa istambul ambalo kwa kiasi kikubwa watalii mbali mbali hufika na kuona mambo mbali mbali ya kihistoria na kumbu kumbu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2011

    Michuzi asante kwa kutuhabarisha. Inawezekana ni matatizo yangu binafsi, je, Tanzania hatuwezi kubadilisha utaratibu wa walinzi wa vingozi wetu wakuu na kufanya kama wenzetu wa Uturuki na kwingineko - kwamba badala ya yule mwanamume ambaye huwa anasimama nyuma ya Rais akavaa suti ya uraia badala ya suti ya jeshi. Mara nyingi huwa ninakereka unapoona picha ya Ma-rais wetu wametembea nje au wametembelewa na wageni wao na katika umati mkubwa kuna mtu mmoja tu aliyevaa kijeshi - naye ni mlinzi wa Rais. Hawa wenzetu kam Uturuki haina maana kuwa Rais hana ulinzi, bali unafanyika kama hivyo mnavyoona pichani - ni ustraabu zaidi. jamani tuige mazuri.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2011

    Nchi nyingi za Afrika zinafata mtindo huu. Haina maana walinzi wenye suti hawapo. Rais halindwi na mtu mmoja, wenye suti pia wapo!! Niliomba muhusika wa hii site angalie "spelling" sio Istambul, bali ni Istanbul. Maoni yangu mengi unayabaniya na wala hayana matusi inakuwaje?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2011

    mdau wa kwanza..huyo sio mlinzi exaclty..ni protocols tu za nchi zetu ndio maana wakati mwingine huyo jamaa huwa anabeba ma file au hotuba ya rais mkononi mwake lakini walinzi wake hawawezi kubeba ma file, wao wanamlinda tu....walinzi au usalama wa taifa huwa wapo pembeni wakiwa in plain clothes pia...mimi binafsi sipendezwi na huu mfumo, sidhani kama unapendeza sana kwa dunia ya leo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...