Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Ali Mohammed Shein amemteua Mheshimiwa Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema kwamba uteuzi huo unaanza leo tarehe 01/05/2011.
Mheshimiwa Rais Dk. Shein amefanya uteuzi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 94(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.Mwezi uliopita, Mheshimiwa Makungu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Aprili 5 mwaka huu, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein alimteuwa Jaji Makungu kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar kwa mujibu wa kifungu cha 94(4) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Jaji Makungu anachukuwa nafasi hiyo baada ya Mheshimiwa Hamid Mahmoud kustaafu kazi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar kwa mujibu wa sheria.
Nafasi nyengine alizowahi kushika ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Tanzania(NEC).
Pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora. Aidha, Jaji Makungu aliwahi kuwa mwanasheria wa Serikali katika Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa muda mrefu.
Imetolewa na:-
Idara ya Habari(MAELEZO)
Zanzibar


Michuzi, hii mbona inachanganya? yaani Omar Othman kateuliwa mara tatu ktk mwezi mmoja!!! April 5 kuwa jaji wa mahakama ya Zanzibar, alafu kaimu jaji mkuu, alafu leo jaji mkuu wa Zanzibar. mbona uteuzi huu wa kushangaza.
ReplyDeleteMichuzi usibane comment zangu!!
ReplyDeleteSwali: Wakristo Zanzibar hawakusoma? Mbona sijawahi sikia hata mmoja kateuliwa kuwa fulani? Tusiimbe usawa wakati sisi wenyewe hatuwezi kuleta usawa.
Na kweli mdau umeuliza swali zuri. Hata mimi niliwahi kujiuliza ki2 kama hiko. Mkuki mchungu kwa binadamu lakini kwa nguruwe mtamu
ReplyDeleteKwa hiyo?
ReplyDelete