Kipa wa timu ya mkoa wa Kagera akidaka mpira huku mshambuliaji wa timu ya mkoa wa Mbeya Gaudens Mwaikimba akijaribu kufunga wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya pili ya michuano ya Kill Taifa Cup 2011 dhidi ya timu ya mkoa wa Kagera uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
TIMU ya soka ya mkoa wa Mbeya, jana iliifuata Mwanza kwenye fainali ya Kili Taifa Cup baada ya kuibamiza Kagera - Lweru Eagles- mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
TIMU ya soka ya mkoa wa Mbeya, jana iliifuata Mwanza kwenye fainali ya Kili Taifa Cup baada ya kuibamiza Kagera - Lweru Eagles- mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
Mbeya imekwenda fainali hizo kupitia kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Gaudence Mwaikimba, na lile la kujifunga la Luhende Charles katika dakika ya 93 baada ya kumalizika zile 90 za kawaida kwa sare ya 1-1.
Bao la Mwaikimba lililopatikana kwa penati baada ya kipa wa Kagera kumwangusha Said Mtupa na mshambuliaji huyo mrefu hakufanya ajizi kufunga na Themi Felix alilifuta kwenye dakika ya 60 kutokana na walinzi wa Mbeya kushindwa kuondosha hatari hiyo.
Kutokana na ushindi huo, sasa Mbeya kutoka Green City wataivaa Mwanza kutoka Rock City katika fainali ambayo inatarajiwa kuwa kali na ya kuvutia itakayopigwa Jumamosi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...