
Mwenyekiti wa Kamati ya uteuzi wa wanamichezo bora wa chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA), Bw. Masoud Sanani akiongea na wanahabari wakati wa hafla ya kukabidhiwa gari la mwanamichezo bora wa mwaka 2010 litalokabidhiwa leo na Makamu wa Rais Dr. Mohamed Ghalib Bilali leo jioni katika hoteli ya Movenpik jijini Dar es salaam. Kushoto ni katibu mkuu wa TASWA Bw. Amir Mhando, kushoto kwa Bw. Sanani ni mwenyekiti wa TASWA Bw. Juma Pinto akifuatiwa na Bi. Teddy Mapunda, Afisa Uhusiano wa Serengeti Breweries

Afisa Uhusiano wa Serengeti Breweries Bi. Teddy Mapunda akimkabidhi Mwenyekiti wa TASWA Bw. Juma Pinto funguo za gari hilo huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo Bi Yasoda (shoto) na Bw. Masudi Sanani

Gari atalokabidhiwa mwanamichezo bora wa mwaka 2010
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...