Mabaki ya basi la kampuni ya Sumry yakiondolewa eneo la tukio huku yakifichwa kwa turubai kama walivyonaswa na camera ya blogu hii ya www.francisgodwin.blogspot.com leo
Haya ni mabaki ya basi hilo na hili ni paa la basi hilo likiwa limetengana na chesesi lake
Na Francis Godwin

Vibaka wamepora mali maiti pamoja na majeruhi wa ajali ya basi la Sumry lenye namba za usajiri T 949 BCT aina ya Nissan Diesel iliyotokea jana eneo la Igwawa wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Katika ajali hiyo watu 15 walikufa papo hapo na mmoja kufia hospitali ya Rujewa wilayani Mbarali huku watu zaidi ya 15 wakijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo.

Baadhi ya majeruhi na ndugu wa jirani na marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo walisema kuwa baadhi ya mali walizokuwa nazo zikiwemo fedha ziliporwa na vibaka waliofika katika eneo hilo ambao baadhi yao ni madereva wa magari yaliyosimama kutoa msaada katika eneo hilo.

Mmoja kati ya ndugu hao aliyejitambulisha kwa jina la Yohana Samson alisema kuwa rafiki yake ambaye amekufa katika ajali hiyo alikuwa na Laptop yake pamoja na fedha zaidi ya shilingi milioni 2 ambazo alikuwa ameziweka katika mkoba huo wa Laptop na kuwa baada ya ajali alijitokeza mtu ambaye alifika kwa ajili ya kutoa msaada na kuondoka na mkoba huo na fedha.

Hata hivyo alisema eneo hilo ambalo ni mbali na mji wa Igawa na ni pori ilikuwa vigumu kwa wananchi wa eneo hilo kufika na kuwa wahusika wakuu wa tukio hilo la wizi ni madereva na baadhi ya wenyeji wachache waliofika kusaidia kuokoa majeruhi .

Majeruhi huyo pia ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo na dereva wa basi hilo la Sumri kutaka kufukuzana na basi la kampuni ya Hood ambalo lilikuwa mbele yao na kuwa kama si kufukuzana huku huenda taili hilo lisingepasuka .

Hivyo alitoa lawama zake kwa Sumatra kutokana na kutoka muda wa dakika 10 kwa mabasi hayo kuanza safari katika stendi kuu ya Arusha na ile ya Mbeya na kuwa ni vema Sumatra kutoa muda wa saa moja zima kwa basi moja kuondoka kabla ya jingine kutoka stendi ili kupunguza ligi kwa mabasi hayo .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi emethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Igawa wilayani Mbarali mkoani Mbeya mpakani mwa mkoa wa Iringa na Mbeya.

Alisema kati ya waliokufa, wanaume ni watano na wanawake ni watano ambao hata hivyo majina yao bado hayajapatikana na maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Wazazi Meta Mbeya.

Aliwataja waliokufa kuwa ni dereva wa basi hilo, Makame Juma, Frolence Kitaule Mwalimu wa shule ya Msingi Ubaruku wilayani Mbarali,Thomas Mchalo Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Wengine Bupe Mwaijumba, Magreth Komba ambaye ni Muuguzi katika hospitali ya wazazi Mbeya pamoja na mumewe aitwaye Kandi Komba.

Alisema watu saba waliokufa katika ajari hiyo bado hawajatambuliwa na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wazazi Meta ambapo ndugu na jamaa hadi kufika saaa 6;30 mchana walikuwa wakiendelea kumiminika katika hospitali hiyo kutambua waliokufa.

Kamanda Nyombi alisema majeruhi 11 wa ajari hiyo wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Rujewa-Mbarali na mmoja katika hospitali ya Ilembula na hali zao zinaendelea vizuri.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Twarib Fakiri, Lupi Mwaipalo, Martine Costantine (25) mkazi wa Moshi, Thadeus Logate (43) Mkazi wa Soweto, Andrew Adolf (6), Ezekiel Adolf ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Meta iliyopo Jijini Mbeya.

Majeruhi wengine ni Riziki Chuwa (25) mkazi wa Mbeya, Erasto Kiwaga (25), mkazi Mbeya, Hassan Mohamed mkazi wa Iringa,Bakari Zayumba mkazi wa Dar es Salaam na Halima Abdallah.

Hata hivyo Kamanda Nyombi alisema chanzo cha ajali hiyo kilitokana na kupasuka tairi la mbele upande wa kushoto. Alisema baada ya tairi kupasuka basi hilo liliseleleka na kuacha njia na kuinduka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2011

    Kwanza pole kwa majeruhi na familia zilizopoteza jamaa kwenye msiba huu.Naomba blog yako michuzi iweke mada kuhusu jinsi ya kupunguza ajali hizi za mabasi "yaendayo mikoani"maana ajali zimefikia kubaya.Ajali haina kinga lakini mimi nadhani kuna tatizo uendeshaji wa mabasi haya kuanzia kwenye usalama wa mabasi yenyewe, wamiliki,madereva,barabara zetu,sheria za barabarani,"trafiki",abiria wenyewe,nk.Serikali mko wapi,mbona haya mabasi yanapoteza maisha ya Watanzania namna hii.Hauwezi kumaliza mwezi au miwili bila kusikia ajali ya haya mabasi.

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2011

    We see a lot of reports like these in the blog. It may be due to selective reporting, for if it is not,then Bongo roads are deadly in deed
    Mungu warehemu na wape imani na faraja waliofiwa
    Wakatabhu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2011

    Watanzania tunatakiwa kureview usafirishaji Tanzania.ni dhahiri ajali zinaepukika kama kuna jitihada za makusudi.ushahidi upo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2011

    Hizi wala hazifai kuitwa ajali(accident) tena. Ajali haina kinga lakini hizi za kweu zina kinga ila uzembewa nchi.

    1. Rushwa kwa police
    2. Uendeshaji mbovu
    3. Maboss hawajali kuangalia magari yao yamefanyiswa service lini
    4. Madereva hawana ujuzi wa kuendesha hayo mabasi
    5. Wanaendesha kwa speed.

    According to the news hii ilitokea baada ya basi kupasuka tire ya mbele. Je alikua anaendesha kwa speed gani, je alikua anajua jinsi ya kuendesha hilo gari au ameshawahi kusoma hata defensive driving, hizo tires zilikua na milage ngapi, huyo dereva alikua ameendesha kwa masaa mabapi bila kupumzika au siku zake za kupumzika ni ngapi kabla ya kufanya safari ndefu kama hiyo, je wanachekiwa kama wanatumia illigal drugs au la?

    Kuna mambo mengi sana ya kuangalia kabla ya kusema ni mipango ya Mungu au ajali haina kinga. Kwa nini iwe Tanzania tu ndio ajali za mabasi ziko nyingi sana? Ina maana mipango Y aMungu ni mibaya kwetu tu?

    Je mabasi haya yanayopata ajali CEO wao wanalipa faini kiasi gani kwa waathirika? Kama hamna ndio maana hawajali hata kuangalia magari yao yakoje kabla hawajaliweka barabarani, madereva wanaujuzi gani na lwa bile police kila siku kupokea rushwa wakiona limejaa sana hawashiakiwi, wakiona lina speed sana hawashitakiwi na mweisho wa yote ndio haya maisha ya innocent people yanateketea.

    Halafu ukiona number ya watu waliokufa wala hamna mtu anayeshtuka lakini just imagine uanze kuelezewa mtu mmoja mmoja kati ya hao waliokufa. Ujue kuna baba, mama, watoto, shangazi, bibi na babu za watu hapo. Unajua ni maisha ya watu wangapi yanaharibika kwa ajili ya uzembe wa watu wachache wenye vitambi mpaka vifungo vya mashati haviwezi kufunga?

    Inabidi watu wanaohusika sio kwenda kanisani au misiktini tu na kuona kuwa wewe ni mtakatifu na Mungu hakuoni. Mungu atakulaani na kukuuliza kazi uliyopewa uliifanya vipi? Je uliwajibika vizuri?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2011

    Mbona nchi zilizoendelea hatusikii mambo haya?watu wanasimamia sheria na anayevunja sheria anachukuliwa hatua kali.kwa nini kwetu imekuwa kama ni kitu cha kawaida?viongozi wetu wanachojua ni kusema 'nimesikitishwa sana na ajalli na kutoa salamu za rambirambi'tutatoa salamu za rambirambi hadi lini?hizi salamu zinamsaidia nini mtoto aliyebaki yatima?kwa nini serikali isijali utu wa watu wake?kwa nini wanaosimamia usalama wa barabarani wasichukuliwe hatua kali?hao watu wanalipwa mshahara kwa kazi gani wanayofanya?yaaaaaaaani sijui nisemeje maana inasikitisha.wasomi wa tanzania mko wapi jamani?rushwa mbaya jamani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2011

    Tairi ye mbele ikipasuka atalaumiwa nani? Mimi ni dereva wa malori tairi inapopasuka gari inaenda inapotaka na ni wrong kumlaumu dereva na mkae mkijua ni split secong decission. Hata kama angekuwa anaenda km 10 kwa saa kama tairi inapasukia Kitonga gari litaingia porini. Siku zilifika tu jamani.
    Oh by the way kwenye ajali hii asilimia kubwa ya waliyopona walivaa mikanda na basi lilivyo bingirika hwakutoka kwenye sit zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...