Waandishi wa habari wakipata kikombe cha dawa yenye uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali kilichotolewa leo jijini Dar es salaam na Mganga kutoka mkoani Mwanza Muhanga Kapeji Hela(mwenye shati nyekundu). Mganga huyo anashirikiana na Taasisi inayojulikana kama Tanzania Medical Plant Foundation (TMF). Mganga huyo ataanza kutoa dawa hiyo jijini Dar es salaam kuanzia wiki ijayo. Kikombe ni alfu (1,000/- ).

Picha na Tiganya Vincent, Dar es salam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2011

    Kikombe nacho kimebaki kuja Zanzibar. Yakhe tuleteeni nasisi basi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2011

    Huu ni upuuzi unaoendelea. Nashangaa hata serikali imesinzia tu. Badala ya kuzuia upuuzi huu kuendelea. Serikali inafurahi sana. Maana badala ya wananchi kuibana serikali kwa kudai kutatuliwa kero yake wanabakia kushabikia kikombe.Laiti kama ningekuwa kiongozi wa wenye vyombo vya habari ningewashauri wamiliki wa vyombo vya habari kukubaliana na kuacha kutangaza UPUUUUZI huu wa vikombe. UPUUZI huu unazidi kuliaibisha taifa letu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2011

    Jinsi gani Watz wameacha kusali sasa hivi wanahangaika na vikombe, subirini ukweli utakapojulikana kuwa hawakutumwa na Mungu ilikuwa mizimu na nguvu za giza, wakati huo umeshakunywa either inagundulika ulikuwa mkojo, kinyesi au hata damu za wale watoto waliookotwa jalalani Dar. Na si vizuri kuwa wa rahisi sana hasa kwenye kitu unachokunywa/kula, wanasema stop and think before.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2011

    ABSOLUTE RUBBISH. HILI NI TAIFA LA WAGONJWA?MBONA KILA ANAPOIBUKA MTU NA MAUZAUZA YAKE WATU WANAKWENDA TU KUPANGA FOLENI?ETI KIKOMBE. HILI NI TAIFA LA WATU WALIOKATA TAMAA?SIJUI MNASEMAJE WANDUGU.
    TAIFA HILI LITAJENGWAJE NA WATU WAGONJWA?ASILIMIA KUBWA - MAGONJWA SUGU. KUANZIA VIONGOZI HADI NA RAIA WAKE?AMA KWELI TAIFA LINATEKETEA. MUNGU IBARIKI TANZANIA, NA UWAPE WATU WAKE HEKIMA NA BUSARA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2011

    you can take the African from the bush but you cannot take the bush from the bush. Huo ndio ukweli, tukitaka tusitake. Michuzi huwa unaibania hii, it is high time watu wajue kwamba bado sisi ni wa bush tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2011

    Tuacheni na vikombe vyetu.

    Mbona nyie mmechomekewa kifo cha Osama na Obama mnahangaika nacho sasa hivi CNN na tv zote kubwa wamebakia kubwabwaja propaganda za Osama kafa sijui tumeingia na helikopta mbili special force navy seal na utumbo mwingine.

    Maiti mpaka kesho haioneshwi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2011

    kwa kwel taifa linamuitaji MUNGU SAANA.wapendwa ktk BWANA yatupasa tuzidi kuliombea taifa letu kwan sasa watu wanamsahau MUNGU MPONYAJI,imani ya watu inaamia ktk vikombe.ooh MUNGU turehemu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2011

    Asante sana bwana mganga kwa kutuletea kikombe Dar,kwani Samunge mbali sana,mwaka huu madaktari na manesi watajibeba.Kinapatikana wapi jamani?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2011

    BAADA YA WATU WENGI NA VIONGOZI KWISHA KUNYWA KIKOMBE CHA BABU NDIPO SERIKARI IKAFANYA UCHUNGUZI WA SIKU MBILI TATU WAKASEMA ETI MAJI YA BABU HAYANA MADHARA. UCHUNGUZI HUO ULIKUWA WA JUU JUU TU KWANI HAUKUANGALIA JE MADHARA YA MUDA MREFU NI YAPI.


    SWALI LANGU NI HIVI JE IWAPO HAWA WOTE WENYE VIKOMBE WAMEKULA NJAMA YA KUGAWA SUMU FULANI HIVI AMBAYO MADHARA YAKE NI KIFO AU KISHIKWA NA KICHAA BAADA YA MIEZI SITA HADI TISA TOKA MTU ANYWE KILICHOKO KWENYE HICHO KIKOMBE; JE ITAKUWAJE? JE TUTAMUDU MISIBA NA HUDUMA KWA VICHAA WETU? JE SI NDIO NCHI YETU ITAKUWA VIONGOZI WOTE HOI NA WANANCHI WAKE PIA TAABANI? ITAKUWAJE JAMANI. HUU ULIMBUKENI WETU KUNYWA KUNYWA TU VITU TUSIVYOVIJUA? WATANZANIA JAMANI

    ALEX BURA, DAR

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...