BENDERA YA TANZANIA IKIPEPEA KWENYE KANISA HILO MAARUFU KWA HISTORIA YA NCHI YA UINGEREZA, HUSUSAN FAMILIA YA KIFALME KAMA VILE NDOA ZA PRINCE CHARLES& DIANA NA WILLIAM & KATE.
MHESHIMIWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, BWANA PETER KALLAGHE (WA NNE KULIA), MKEWE MAMA JOYCE KALLAGHE ( WA TATU KULIA), MAMA BERTHA KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NCHI ZA NJE TANZANIA(DIASPORA DESK) WA NNE KUSHOTO), BAADHI YA MAOFISA WA UBALOZI, VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA HAPA LONDON, WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUMALIZIKA KWA IBADA KUIOMBEA NCHI YETU TANZANIA. IBADA HIYO AMBAYO HUFANYIKA KILA MWAKA KATIKA KANISA HILO, HUANDALIWA NA KANISA HILO LA WESTMINSTER ABBEY. KANISA HILO LIMEKUWA LIKIAANDAA IBADA KWA KILA NCHI AMBAZO NI MWANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA (COMMONWEALTH COUNTRIES) MARA ZINAPOFIKA SIKU ZA UHURU WA NCHI HIZO.
BAADHI YA MAOFISA WA UBALOZI, VIONGOZI WA JUMUIYA MBALIMBALI ZA WATANZANIA HAPA UINGEREZA NA MARAFIKI WA TANZANIA, KWENYE PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUMALIZIKA KWA IBADA MAALUM YA KUIOMBEA NCHI YETU TANZANIA, IBADA AMBAYO HUFANYIKA KILA MWAKA, ILIANDALIWA NA KANISA LA KIANGLIKANA LA WESTMINSTER ABBEY SIKU YA JUMATATU TAREHE 09 MEI 2011.

SAHIHISHO: Inaitwa "Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa" si ""Nchi za Nje"", In English "Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation"...Ni kosa linalojirudia mara kwa Mara hata kwa wahusika wa Wizara yenyewe.
ReplyDeleteBalozi leo naona uko na Wife.Ulimwacha wapi kwenye ile Royal Wedding