Leo ni siku ya pili nikiwa ninahangaika kujaza form ya mkopo ya elimu ya juu katika website ya HESLB kwenye link yao ya OLAS, Mdogo wangu ambaye amemaliza kidato cha sita aliniomba nimsaidie kujaza zile form kwani yeye hakuwa familia na technologia, kwa kuwa ninatumia mtandao ambao unasadikiwa kuwa na kasi zaid na cheap sikusita kumsaidia , lakini yaliyonikuta nimebidi kuandika haya.

Ndugu yangu michuzi kuload page moja ili uweze kujaza utarudia zaidi ya mara tano na utajibiwa message hii kama unatumia google chrome

Oops! Google Chrome could not connect to olas.heslb.go.tz

Try reloading: olas.­heslb.­go.­tz

Additional suggestions:

· Access a cached copy of olas.­heslb.­go.­tz

· Go to heslb.­go.­tz

· Top of Form

Search on Google:

hii message unakumbana nayo kila mara kutoka page moja kwenda nyingine, mimi nilikomaa kwa siku ya jana mpaka nikafika page hii

Application Fee Payment Details Update

Applicants MUST provide TRUE INFORMATION for the fee payment. This information shall be counterchecked with Mobile Payment Systems. Provision of FALSE or FORGED information is a CRIMINAL OFFENCE. ANY ATTEMPT to cheat may result into being DENIED A LOAN as well as facing LEGAL ACTION.

Service Provider *:

Transaction Id *:

Amount Paid *:

Your Password *:

* means MANDATORY Field

hapa si nikajaza detail nilizokuwa nazo za M-Pesa, baada ya attempt kama tano ikafanikiwa kuload he!!! baada ya hapo si ndo nikastack message iloniletea ndo hii

A Database Error Occurred

Error Number: XXXX

Duplicate entry 'XXXXXXX' for key 2

INSERT INTO `feepayment` (`pdate`, `provider`, `amount`, `transid`, `registerid`) VALUES ('2011-05-04', '1', '2', 'XXXXX', 'XXXX')

hapo kwenye XXXXX nimetoa details isije ikala kwangu

ikiwa mimi napata matatizo kama haya nikiwa atleast nina idea na hii technologia wale wenzangu je kama tatizo ni server capacity iongezwe au kama ni transmision ifanyiwe marekebisho

mdau DSM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2011

    yaani hauko peke yako,tangu juzi najaribu kujaza nashindwa.jana wakasema mtandao uko kwenye marekebisho, kwenye sehemu ya kuchagua mkoa haitoi options za miji.ilimradi karaha tuuuu..muda unaenda,watu hatufanikiwi kujaza..wahusika hebu waangalie hili swala

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2011

    badili browser!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2011

    Jaribu kutumia browser nyingine. Nimejaribu kuingia kutumia IE9, safari, na mozila fox ili kuangalia imeingia bila matatizo. Jaribisha kutumia browser nyingine labda utafanikiwa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2011

    mdau uliyepata kwikwi yani mdogo wako anaingia chuo kikuu haweza kujaza maombi ya mkopo online?? Kazi ipo!!? Hii inaonyesha ni jinsi gani elimu ya tanzania ilivyo duni!! Sijui kama ataweza kushindana duniani maana sasa watoto wa chekechea kwenye nchi zilizoendelea wanafanya mtihani online

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2011

    tatizo mtandao unazingua,sio kwasabau watu hawajui kutumia computer!!nimejaribu chrome,safari,explorer tec zote zinanipa tatizo hilohilo,hata computer piz nimebadilisha lakini tatizo haliishi

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2011

    Hapo kuna tatizo la system (A Database error has...), yaani kuna bug. Programmer alisahau kuchek kama mtumiaji atajaribu kuingiza details zilezile mara 2, ndo maana zinatokea message za kwenye database. Kilichotokea ni kwamba ulipo-reload(refresh), data zilikuwa zimeshatumwa na baada ya ku-reload zikaenda tena. Ilitakiwa programmer aonyeshe kuwa umeshafanya transaction. Sio ishu saana maana ndo kwanza system inaanza kufanya kazi, ni kawaida kwa software zozote kuwa na bug (hata za 'famous' Microsoft).

    Usijali sana maana kwa mujibu wa huo ujumbe ni kwamba taarifa zako zimeshahifadhiwa kwenye database ya OLAS.

    Tatizo la awali (Ooops Google chrome...) linasababishwa na aidha poor network connection (net inakata mara kwa mara), server ya OLAS iko busy sana,au tatizo la browser, Unaweza pia ukapata same msg kama umekosea address (which is not the case presently).

    Suluhisho ni moja: kwa bodi kuongeza download speed kwenye server(OLAS), watumiaji wajaribu aina nyingine za browser (e.g Firefox,Opera), na kutumia network reliable connection (mfano kwa walio dar wanaweza kwenda posta mpya azikiwe-net ya posta ni nzuri).

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2011

    we mdau hapo juu acha upuuzi na dharau.mwenzenu kaomba msaada baada ya kusumbuka na hiyo blog,badala ya kumsaidia wewe unaanza madharau yako,ndiyo tukuone umeendelea wewe,aah aibu yako.

    Big up kwa wote mliotoa mawazo mazuri huenda akijaribu browser tofauti yaweza saidia.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2011

    mimi kinacho niuma ni ninapo kumbuka uzinduzi wa mkongo sijui mkonga,.. wa masiliano zilotolewa ahadi na mbwembwe kibao na mkuu wa kaya.., nafikiri ni mwaka sasa umepita toka uzinduzi lakini kasi ya internet kila siku ni afadhali na jana... wadogo zetu wana hangaika kujaza fomu za mkopo za kuomba chuo wanatumia gharama kubwa kwenye mainternet cafe,.. dah jamani hivi nani katuroga ?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2011

    Asante mdau ulietoa maelezo ya kiutaalam. Nasi tusikatishe tamaa taasisi zetu zinapojaribu kupiga hatua. Tunapohitaji kupiga hatua fulani ni lazima tuanze sehemu fulani ambayo tunaamini wakipata maoni yaliyo bora tutasonga mbele badala ya kusema hiki hakifai.
    Unayesema watoto wadogo wanajua computer fikiria tena na tena ulikotoka usifikiri hao wamefika tu huko juu hadi watoto wao wadogo wanajua wanachojua. Hata tukikuuliz umetoka wapi na huko kijijini kwenu ni watoto wangapi basi umewasaidia watumie computer kufanya mitihani. TUNAHITAJI TUKUSAMEHE MAANA HUJUI ULISEMALO!! POLE SANA

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 06, 2011

    huyo ana ulimbukeni wa kukaa nje ya Tanzania

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2014

    Jamani nikifanya registation napata hii message nisaidieni tatizo linaweza likawa ni data nilizoingiza au OLAS

    A Database Error Occurred
    Error Number: 145

    Table './olas/users' is marked as crashed and should be repaired

    SELECT * FROM (`users`) WHERE `f4indexno` = 'S5222.0001.2011' LIMIT 1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...