Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa,Omben Sefue

Kwa Juma zima Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, naibu wake, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, wahisani , wawakilishi kutoka nchi tajiri , mashirika, jumuiya za kijamii, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na nchi masikini kabisa duniani walikusanyika mjini Istanbul Uturuki ili kutanabahi mbinu za kuzisaidia nchi hizo masikini kabisa kuondokana na hali hiyo iliyomea mizizi.

Mkutano huo umejadili kwa nini nini cha kufanya, hatua walizopiga tangu mkutano wa Brussels miaka 10 iliyopita na nini kifanyike katika miaka 10 ijayo kuhakikisha nchi hizo fukara kabisa 48 ninapungua japo kwa nusu katika miaka 10 ijayo. Nchi hizi zimeelezwa kughubikwa na umasikini wa kupindukia, uongozi mbomu na miundombinu duni.

Katika kuhitimisha mkutano huo ijumaa hii uliofungwa na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose- Migiro wadau wameafikiana kwamba sekta binafsi zitahitaji kuchukua jukumu kubwa hasa katika kuwekeza , lakini pia serikali hizo ambazo nyingi ziko Afrika Kusini kwa jangwa la Sahara zina wajibu wa kutimiza kama amesema Cheick Sidi Diarra katibu anayehusika na nchi hizo maskini kwenye Umoja wa Mataifa.

Na mataifa tajiri yamekumbushwa kutekeleza ahadi zake za msaada kwa nchi masikini ambao ni sawa na asilimi 0.2 ya pato la taifa. Nchi Masikini zenyewe zinasema zilikwenda kwenye mkutano huo na malengo na zinaondoka na ahadi ambazo zinatumai zitawasaidia.Kutathimini matarajio ya nchi maiskini nmkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha amezungumza na balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Omben Sefue aliyehudhuria mkutano huo.

Kusikiliza makala hii bobya hapa

http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/
au
http://www.facebook.com/UNRadioKis

http://twitter.com/redioyaum

au moja kwa moja kwenye mahojiano yenyewe

http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2011/05/mkutano-wa-um-waainisha-mipango-ya-kuzikwamua-nchi-masikini-kabisa-dunianisefue/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...