Sehemu ya milima ya Kitonga katika picha
Habari toka Iringa zinasema kuwa usiku kuamkia leo kundi kubwa la majambazi wakiwa na silaha walifunga barabara kuu ya eneo la mlima wa Kitonga na kuteka magari zaidi ya 20.
Habari zinasema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 8 usiku na kudumu kwa zaidi ya saa 1 baada ya baadhi ya madereva kupiga simu kituo cha polisi mjini Iringa ambao walituma askari polisi wa kituo cha Ilula ambao walifika kwa wakati kunusuru usalama wa madereva ambao walikuwa wametekwa.
Mmoja kati ya madereva aliyenusurika katika tukio hilo aliueleza mtandao huu kuwa yeye alikuwa na gari jipya lenye namba za IT akitokea Dar Dar es Salaam kwenda Tunduma mkoani Mbeya akiwa na wenzake ambao walitangulia na kukumbwa na mkasa huo.
Dereva huyo alisema yeye na baadhi ya madereva walipoona hali hiyo walirudi nyuma hadi Hotel ya Kitonga majira ya saa 10 usiku baada ya polisi kufika eneo hilo na kuwatawanya majambazi hayo na kuwahakikishia usalama madereva hao japo alidai kuwa usafiri wa katika barabara hiyo ulisimama kwa masaa kadhaa wakihofia kupita eneo hilo.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangala kwa ajili ya kupata idadi kamili ya magari yaliyotekwa na madhara yaliyojitokeza zinafanywa na mdau Francis Godwin www.francisgodwin.blogspot.com

Kitonga kujengwe vituo viwili au vitatu vya polisi na wawe wanafanya doria mara ka mara ktk barabara hiyo.
ReplyDeleteKitonga is the beutifull and attractive site for thugs of all kid!I wonder why our security system didnt notice that to put 2 police post!!
ReplyDeleteHata vingejengwa vituo mia moja(100) haisadii kitu. Tatizo kubwa ni kwamba polisi wanashirikiana na majambazi katika kuhujumu wananchi. Hili ndio tatizo kubwa sana.
ReplyDelete