Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Msaidizi wa Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Modest Mero, baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Ataturk jijini Istambul jana. Makamu wa Rais yuko nchini Uturuki kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Umoja wa Matifa unahusu maendeleo ya nchi maskini, Mkutano huo unaanza kesho na kumalizika Mei 13, 2011. Katikati ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Dkt. Mbaraka Lijohiy, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Ataturk, Istanbul jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Sundery baada ya Dkt. Bilal kuwasili mjini Istambul jana. Makamu wa Rais yuko nchini Uturuki kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Umoja wa Matifa unahusu maendeleo ya nchi maskini, Mkutano huo unaanza kesho na kumalizika Mei 13, 2011. Kushoto ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal,akiongozana na mkewe Mama Zakhia Bilal na baadhi ya viongozi alioongozana nao baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Ataturk, Istanbul jana Mei 7, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya nchi maskini.
Makamu wa Rais, akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Mbaraka Ljohiy, ambaye ni Mkurugenzi wa Plastic , Reconstructive, Esthetic Had and Microsurgeory (kulia) na mfanyabiashara aishie nchini Uturuki, Ally Kilumba baada ya kukutana nao jana alipowasili jijini Instanbul, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya nchi maskini. Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2011

    SAFARI ZA UTURUKI MBONA NYINGI SANA SIKUIZI?
    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2011

    Makamu wa rais anawakilisha na kuongoza ujumbe wa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...