
Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christine Kamuzora (kulia), akielezea faida ya kujiunga na mfuko huo katika semina ya elimu ya umma kuhusu NSSF iliyowahusisha wanachama wa kikundi cha wajasiliamali cha akina mama wa Ubungo cha MUWASIDA SACCOS Dar es Salaam wikiendi hii. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinda

Mwanachama Hidaya Mohamed wa kikundi cha wajasiriamali cha akina mama wa Ubungo cha
MUWASIDA SACCOS akiuliza swali kwa mwendesha mada kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakati wa semina ya elimu ya umma kuhusu mfuko huo

Mwanachama wa kikundi cha wajasiliamali cha akina mama wa Ubungo cha MUWASIDA Saccos, Editha Rimoy akisoma kijarida cha mafao ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alichopewa wakati wa semina ya elimu ya umma kuhusu mfuko huo

Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mwanakombo Mohamed akigawa mfuko wenye fulana, kofia na vijarida vya NSSF kwa wanachama wa kikundi cha wajasiriamali cha akina mama wa Ubungo cha MUWASIDA Saccos,waliohudhuria semina ya elimu ya umma kuhusu mfuko huo, Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...