Na Woinde Shizza,Arusha

Zaidi ya Makatibu Muhutasi 1500 wanatarajia kuhudhuria uzinduzi wa Chama cha makatibu muhutasi Tanzania (TAPSEA ) kinatarajiwa kuzinduliwa kesho kikiambatana na kongamano kubwa litakalo fanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa mwenyekiti wa chama hicho, Pilli Mpenda alisema kuwa nia haswa ya kuanzisha na kuzindua chama hicho ni kuweza kuujulisha umma wa Tanzania kuhusu uwepo wa chama hicho na majukumu yake kwa ujumla.

Alisema kuwa uudwaji wa chama hichi umetokana na ukweli kwamba licha ya juhudi mbalimbali za kuwakutanisha wanataaluma wa fani ya ukatibu muhtasi lakini bado haijawezekana kuwa na chombo chochote kinachosimamia maslahi ya makatibu muhtsi (wahazili) hapa Tanzania mbali ya waajiri.

Alibainisha kuwa kwa kipindi hichi cha sasa hivi kumekuwepo na wahazili wengi ambao wamekuwa hawafuati sheria na wamekuwa wanakiuka misingi ya taaluma na maadili kwa ujumla hivyo chama hichi pia kitatumika kwa ajili ya kuzuia vitondo hivyo.

Mpenda alisema kuwa fani hii ya fani hii ni kama zilivyo kama fani zingine kama wanasheria ,madaktari ,waandisi na hata wanahabari hivyo inapaswa kuongozwa na miiko ambayo lazima vilindwe ,viendeleze na kuboreshwa ili kuweza kwenda sambamba na mabadiliko ya uchumi na kijamii,utandawazi pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

"pia shabaha ya chama hichi ni kubwa ni kuwafanya wahazili wahamasike kubadilika sambamaba na mabadiliko ya sayanzi na teknolojia pamoja na waweze kujiendeleza kielimu na wajiongezee ujuzi na maarifa ili waendane na mabadiliko yanayotokea hapa nchini"alisema mpendwa.

Alitoa wito kwa watu ambao wanafanya kazi hii na wamesomea fani hii waieshimu fani na kuendeleza na kulinda hadhi ya kazi ya uhazili pamoja na kila mmoja kutoa ushauri wa kitaalamu wa uahazili.

"nia pia ya cha hichi ni kuwakutanisha wahazili mara kwa mara ili waweze kukjadili maendeleo na matatizo ya taaluma yao pamoja na kutafuata mbinu mbadala za kuyatatua na kuwawezesha kufahamiana na kujenga ushusiano wa kitaaluma"alisema Mpenda.

Aidha alisema kuwa kauli mbiu ya kongamano la makatibu muhtasi kwa mwaka 2011 inasema kufanya mapinduzi /kuhuisha miiko yetu mahala pa kazi.

Alisema kuwa chama hicho pia kitasaidia kuwathibiti wafanyakazi muhtasi ambao wanakiuka sheria za kazi yao na kuvujisha siri mbalimbali za ofisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    Nawashukuru makatibu muhtasi wenzangu mliokuwa na mawazo mazuri kuhusu kuanzishwa kwa chama chetu cha Makatibu Muhtasi. Ombi langu ni kwamba tunafikiria nini kuhusu suala la kupanda kwa ada ya mafunzo ya uhazili mnalionaje, maana gharama ni kubwa ukilinganisha na mshahara tunacholipwa, na hapohapo kuna baadhi za ofisi kama kuna safari, mikutano ya kikazi mabosi hawawashirikisha Makatibu muhtasi wao, wanawachukua watu baki, je utunzaji wa siri za ofisi utakuwepo. Tujaribu kulichunguza suala hili, mabosi nao wanatakiwa kupata elimu kwamba siri zao za ofisi wasiwe wanawaambia wengine ambao hawana uvumilivu wa kutunza siri, maana na wao wanachangia katika uvujishaji wa siri, lakini mambo yakiharibika Katibu ndio unapata lawama. Huu ni mtazamo wangu, kwamba ukifuatilia ofisi ambayo inalalamika kwamba siri za ofisi zinavuja utagundua kuwa wajumbe wanaoshirikishwa katika vikao eidha vya ofisi baadhi yao wakishatoka katika vikao hivyo wanaanza kujadili yale yaliyojadiliwa na watu wasiohusika.
    Kwa hiyo hata na sisi inabidi tujitazame ili kujua nini chanzo cha kuvuja kwa siri za ofisi.

    Asanteni, nawatakia kazi njema na mwendelezo mwema wa chama chetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...