Balozi wa Misri nchini Tazania Bw. Wael Adel Nasr (kulia) akimkabidhi mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema vifaa vya matibabu na dawa zenye thamani ya dola za Marekani laki tano ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 700 kusaidia huduma za afya katika hospitali ya jeshi la polisi kikosi cha Afya makao makuu (Kilwa Road)ambayo huhudumia familia za askari na wananchi leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Misri nchini Tanzania Bw. Wael Adel Nasr akiongea na viongozi na watendaji wa jeshi la Polisi nchini wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya matibabu na dawa kusaidia huduma za afya katika hospitali ya jeshi la polisi kikosi cha Afya makao makuu (Kilwa Road) leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema(katikati)akishirikiana na Kamishna wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la Polisi - CP Clodwing Mtweve na Balozi wa Misri nchini Tanzania Bw. Wael Adel Nasr (kushoto) kuimba wimbo wa Maadili ya Afisa wa Jeshi la Polisi leo wakati wa hafla fupi ya kupokea vifaa vya matibabu na dawa kutoka ubalozi wa Misri.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu vifaa vya matibabu na dawa zilizotolewa na nchi ya Misri kusaidia huduma za afya katika kituo cha afya cha Jeshi la polisi Kilwa Road, kushoto kwake ni balozi wa Misri Bw. Wael Adel Nasr.
Kikundi cha ngoma za asili cha Jeshi la Polisi kikitoa burudani leo wakati wa hafla fupi ya ya Jeshi la Polisi kukabidhiwa vifaa vya matibabu na dawa kutoka ubalozi wa Misri nchini, tukio lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wageni, askari na maafisa wa Jeshi la Polisi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla fupi ya Jeshi la Polisi kupokea vifaa vya matibabu na dawa kutoka ubalozi wa Misri leo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...