Mpiganaji Richard Mwaikenda
MPIGAPICHA Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, ambaye pia ni Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda ameporwa begi lenye kamera na kompyuta na vibaka waendesha pikipiki.

Vibaka hao waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki,walimpora begi hilo lililokuwa kiti cha mbele cha gari lake alilokuwa akiendesha, likiwa karibu na makutano ya barabara za Kitunda na Nyerere, eneo la Banana, Ukonga, Dar es Salaam Jumamosi wiki iliyopita.

Aliyechukua begi kwenye gari ni kibaka aliyepakizwa nyuma na pikipiki hiyo kuondoka kwa kasi kuelekeaUkonga na kumwia vigumu mpiga picha huyo kuachia usukani kuwafukuza kwani magari yalikuwa yameanza kutembea. Alitaja vitu vingine vilivyokuwemo kwenye begi hilo kuwa ni, Modemu ya Vodacom, kifaa cha kutolea picha kutoka kamera ya digito kwenda katika kompyuta (Cardreader),Flash, vitambulisho vya kazi na nyaraka muhimu.
Akisimulia tukio hilo, Mwaikenda alisema , inaelekea vibaka hao walimfuatilia kutoka Kitunda ambapo alisimamisha gari lake na kuchukua kamera kwenye begi na kupiga picha mashimo makubwa barabarani karibu na Kituo Kidogo cha Polisi cha Kitunda. 

Mwaikenda alikuwa anatokea nyumbani kwake, Kivule kwenda Pugu Kanisani kuripoti tukio la Ibada ya misa ya shukrani kwa Hayati Papa John Paul wa Pili kutangazwa Mwenye Heri.Ibada hiyo iliongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Mwaikenda ameshatoa tarifa Polisi juu ya wizi huo wa kutumia pikipiki ambao umekithiri katika miji mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. POLE SANA NDUGU YANGU. NI MATATIZO HAYA YANAWEZA MKUTA MTU YEYOTE. ISHUKURIWE WEWE MWENYEWE HAUKUDHURIKA

    ReplyDelete
  2. jembeulayaMay 29, 2011

    Pole sana ila kwa vile wewe ni mwanahabari ingekuwa vema ukaripoti habari kamili ili kurahisisha ama kusaidia wanajamii kukusaidia kupata mali zako ama kukamatwa kwa wahalifu, aina la laptop, jina la camera, wasifu wa wahalifu, jina la pikipiki, namba ya pikipiki nk, kwa wenzetu huku mbele inakuwa second nature kuchukua taarifa hizi muhimu mfano wasifu wa mhalifu namba za gari nk hii inawapa wepesi wananchi na polisi kuwanasa wahalifu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2011

    Mchangiaji wa mwisho, umeshauri vizuri mno, lakini Kaka, Tanzania sorry Tanganyika hakuna Polisi wa hivyo, askari wetu ( pamoja na wengine kuwa wamesoma) ni mtulinga kwa kwenda mbele. Hawana hata chembe ya akili ya kufikiri, ukitaka jambo lako walichukulie umakini unatakiwa kuwa Mtu mwenye wadhifa, pengine ndiyo maana watu hutaka kuwa viongozi na wala hawataki kujiuzulu hata wakikosea kwani watakosa ULINZI wa vyombo vya dola.
    Mwaikenda nakushauri ukipata lap top nyingine waone wale wataalamu ambao wana maarifa ya kujua iko wapi na inatumika na nani, walishajitangaza sana, pia usiache kuiwekea neno la siri pale tu iwashwapo.
    Pole brother, mimi niliibiwa lap top kwenye basi nikitoka Moshi kuja Dar, Polisi hawakunisaidia lolote, yaani unaweza ukatenda kosa kwa kuripoti kosa Polisi.Makondakta wa Mabasi ya ARUSHA - DAR wanashirikiana na wezi , hili liko wazi na hata askari wanajua , sasa jiulize kwanini bado wizi unaendelea?????????????????? Halafu wnakushangaa kwa kukuambia ULIKUWA HUJUI??? Njia hii ina wezi sana wa Lap top, askari akisema hivi ANAMAANISHA nini???? Kuwa ANJUA na ANASHIRIKI, kwani ndiyo uhai wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...