Mtoto Glory anavyoonekana sasa

Kaka Michuzi,
Habari za maisha na pole na shughuli za kila leo. Hapa nataka msaada wa kuokoa maisha ya Malaika huyu. Anaitwa Glory na ana umri wa miaka mitatu (3). Glory alizaliwa vizuri tu lakini ghafla akaanza kuumwa kama anavyoonekana kwenye picha. 


Hali yake inazidi kubadilika kadri muda unavyoenda. Kama unavyojua matibabu ya nyumbani Tanzania yalivyomagumu. Kwa msaada wako, tunatarajia kumsafirisha Glory India. Gharama za matibabu ni kubwa mno hivyo tunaomba msaada wowote ule. Kwa aliye tayari, piga simu hii;
+255 754 39 7272 
kwa mama yake huyu mtoto.
Mbarikiwe nyote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2011

    uncle tutaftie account yake nasi tuchangie kidogo!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2011

    Tunaomba nambari za simu za mama wa mtoto Glory anayeomba msaada kwenye globu ya jamii. Ahsante, Mdau Ughaibuni

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2011

    Nendeni wizara ya Afya hara sana ili mtoto apewe refereal ya kwenda India kwa ajili ya matibabu zaidi. Cha muhimu pale ni kuwa na referal letter ya kutoka Muhimbili inayothibitisha kwamba mtoto anatakiwa matibabu zaidi nchini India. Kuna budget kabisa kila mwaka hapo wizarani kwa ajili ya matatizo kama hayo na kwanini huyo mtoto asisaidiwe haraka na kupata matibabu muafaka!
    Mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2011

    Mdau, kwanza nataka kutanguliza pole zangu kwa mpendwa mzazi wa Malaika huyu. Pili mdau ningependa kuchangia chochote katika uwezo wangu nlio nao, mimi ni mwanafunzi ambaye nasoma india, naomba kama itawzekana Mungu akijali akafika huku, ningeweza kutuma chochote kidogo Mungu atakacho nibariki nacho kwa ajili ya mdogo wetu Glory. Nafanya hivi kwa sababu huku ni vigumu kutuma hela nje ya nchi nikiwa kama foreigner, naomba Mungu akijali na kufikishwa huku, naomba nijulishwe hata kidogo nilicho nacho kiweze kumsaidia mdogo wetu.

    Mimi ni mtanzania, namba yangu ya mawasiliano ni +91-97808-18694 na Email yangu ni mutta85@hotmail.com.

    Mungu awabariki sana na nia yetu wote kwa mtoto huyu, au mdogo wetu huyu itimie. Amen!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...