Kutokana na uvumi na matamko mbalimbali kutoka kwa wanachama na baadhi ya wasemaji wa Chadema juu ya waanzilishi wa CCJ. Mimi niliyekuwa Mwenyekiti na mwanzilishi wa CCJ Taifa, napenda kufafanua kama ifuatavyo.

A. KUANZIOSHWA KWA CCJ
Kirefu cha CCJ ni Chama Cha Jamii ambacho kilianzishwa na baadhi ya wananchi wa Tanzania. Chana hiki kilipata rasmi usajili wake wa muda, Machi 2, 2010.

Viongozi waanzilishi walikuwa ni:-
1. Ndugu Richard A. Kiyabo- Mwenyekiti Taifa
2. Ndugu Renatus Muabhi- Katibu Mkuu.

Kutokana na taratibu za usajili wa vyama vya siasa hapa nchini ilibidi tuanze harakati za kutafuta wanachama, tunashukuru kwamba Watanzania wengi walituunga mkono na hata kujiunga na chama chetu, na hatimaye kufikia kupata usajili wa muda, na miongoni mwa watu waliojiunga na chama chetu ni pamoja na Mh. Frederick Mpendazoe.

Mpendazoe alitaka awe Mwenyekiti wetu wa Taifa lakini hatukukubali ombi lake ambalo hakuliwakilisha kimaandishi bali kwa mdomo tu, lakini aliapishwa na chama kuwa msemaji wa CCJ.

Waheshimiwa ambao Mpendazoe anadai walikuwa waanzilishi wa CCJ, hoja hiyo ni ya utata mkubwa maana CCJ haikuwahi kuwa na waanzilishi wa aina hiyo yaani:-
1. Mh. Nape Nnauye
2. Mh. Harison Mwakyembe
3. Mh. Samwel Sitta na
4. Mh. Ezekiel Mwabalaswa

Swali la kumuuliza Mh. Mpendazoe ni je alipotangaza kutoka CCM waliompokea CCJ walikuwa hao aliowataja? na je wao walikuwa na nyadhifa zipi na kadi namba ngapi za uanachama? Je amesahau kuwa alinukuliwa na vyombo vya habari akimkaribisha Mh. Sitta kwamba ajiunge na CCJ? hilo atasemaje? Someni gazeti la Mwanachi, ISSN 0856-7573 Namba 03580 la April 6, 2010.

Napenda kuwakumbusha wanasiasa hasa wa Chadema kwamba siasa za udaku hazitawafikisha Ikulu, Watanzania ni waelewa na wala siyo mbumbumbu kama ambavyo Chadema wanajaribu kuonyesha.

Nawakumbusha kwamba Watanzania wamekua kisiasa ndiyo maana hawakuwaingiza IkuluChadema kwa kura zao. Kupigiwa makofi kwenye mikutano ya hadhara siyo kupewa kura kwenye chumba cha kupiga kura, Watanzania wanaelewa kwamba akili za kuambiwa kwenye mkutano changanya na zako kwenye chumba cha kupiga kura.

Nawashauri Mpendazoe na wenzake wa Chadema waache siasa za udaku, Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika si udaku.

Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila kukicha mwisho tutaanza kuamini kwamba pengine hiyo ndiyo sera ya chama chao isiyo rasmi kimaandishi

Kama hawana la maana la kuwaambia wananchi ni bora wakanyamaza kuliko kuwahutubia wananchi uzushi tu kila kukicha.

B. CHADEMA NA HARAKATI ZA PEOPLES POWER
Chadema wameonyesha kuwa nguvu ya umma si kura tena, bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani. wao wanajiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, ajabu wanayotenda siyo ya kidemokrasia tena bali ni kuwa sasa Chama chao ni cha maandamano na vurugu.

Je Wanaiheshimu kweli Demokrasia? Wakumbuke kwamba serikali iliyopo madarakani iliwekwa na Watanzania kwa kura zao sasa kwa nini hawawaheshimu Watanzania?

Wasidhani kwamba demokrasia ya kweli nchini ni mpaka Chadema ishinde uchaguzi. La Hasha! Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura zao.

Huu ni wakati wa kujengaa taifa letu tukishirikiana na Serikali yetu, na si wakati wa vurugu, maandamano kila kukicha, Watanzania tuwe makini na Wanasiasa wasio utakia mema utaifa wetu na amani ya nchi yetu.

Tukumbuke kwamba suala na amani ni sawa na nyanya, nyanya ikitumbuliwa kuishona tena haiwezekani. bila amani shughuli za kimaendeleo haziwezi kufanyika na hata shughuli zao wenyewe Chadema hawataweza kuzifanya.

Maisha ya wananchi kwa ujumla wake yanategemea amani katika nchi, hivyo sisi Watanzania hatuna budi kulipa kipaumbele suala la amani na maendeleo ya nchi yetu. Maneno yetu wanasiasa yawe ya kujenga na wala si ya kubomoa amani yetu, na tujifunze kuwa wakweli badala ya kuendekeza siasa za udaku.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Richard A, Kiabo
Kada wa Chama Cha Mapinduzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2011

    uongo unasaidia nini?

    ReplyDelete
  2. Hakuna atakaye furuga amani ila tu itakae mgusa tu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2011

    Mheshimiwa nadhani hoja ya Mpendazoe hukuipata vizuri. Madai ya Mpendazoe ambayo yameripotiwa katika vyombo mbalimbali ni kuwa hao aliowataja hawakupata kujiunga na CCJ ila walishiriki katika mchakato wa uanzishwaji wake tu na baadae wakaachana na mpango wakuingia CCJ. Sasa unapohoji Mpendazoe aeleze namba za kadi za uanachama wa hao aliowataja ni kitu kisichowezekana. Na pia uthibitisho wa magazeti kuwa Mpendazoe alitoa habari magazetini ya kumtaka Sitta ajiunge na CCJ hauna msingi wowote hapa. Zaidi sana unaweza kuunga mkono tu hoja ya Mpendazoe. Lakini yaonekana pia maelezo yako yanapingana na ya Mh. Sitta katika majibu yake dhidi ya kauli ya Mpendazoe. Kimsingi Mh.Sitta alieleza kuwa suala la mwanasiasa anayekubalika kuombwa kujiunga na vyama mbalimbali ni la kawaida, na mazungumzo ya aina hiyo ni siasa. Na kuwa kwakupima mambo mbalimbali hakuona sababu ya kujiunga na CCJ. Ni vizuri ukafuatilia magazeti ya jana au juzi kama sitakuwa nimekosea, utapata taarifa hiyo.

    Mi nadhani tusiongee kwasababu yakuongea tu au kuonekana tunapinga hoja fulani au kukubaliana nayo pasipokuwa na misingi yakufanya hivyo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2011

    Namshangaa Bw. Kiabo namna ambavyo anakuwa kigeugeu na kutaka kutuaminisha kuwa umma wa watanzania umesahau harakati za CCJ katika kipindi hiki cha mwaka mmoja tu sasa. Watanzania wanafahamu fika kuwa Kiabo hakuwa 'master mind' katika mchakato mzima wa kuanzisha CCJ, bali kulikuwa na kundi kubwa la waCCM waliokuwa wanajiandaa kuhamia CCJ. Kilichobaribu mambo ni ule uharamia uliafanyiwa Kiabo pale Kariakoo na kuporwa briefcase iliyo kuwa na documents muhimu za CCJ. Na hicho ndicho kilichotumiwa kutengeneza wanachama na kadi feki waliosababisha zoezi la uhakiki wa wanachama kuvurugukika. Pamoja na Bw. Kiabo kurudi CCM baada ya kukosa alternative ukweli utabaki ukweli kuwa CCJ ilikuwa imeanzishwa na kundi la wanaCCM waliotaka kujiengua.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2011

    Kinabo kaka yangu pokewee. Mradi wako ccj uliisha salama. Wakimalizana nawe utakuwa mgeni wa nani ?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2011

    Ndo siasa za Bongo hizo!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2011

    Kiabo ni muongo!!!. CHADEMA si chama cha vurugu kama anavyotaka kuwahadaa watanzania. Ni chama kinachoongea ukweli halisi kuhusu jitihada duni za waliopo madarakani katika kuwaletea watanzania maendeleo. Uzuri watanzania siku hizi tumeelimika. Tuna uwezo wa kuchuja kauli na kujua ukweli ni upi na uongo ni upi. Mengi wanayosema chadema si uongo ni kweli tupu. Yapo machache wanayotia chumvi. tunayajua na hatuyaungi mkono. KIYABO KAA KIMYA ACHA WATANZANIA WENYEWE WAAMUE HATIMA YA MAISHA YAO.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2011

    mnategemea aongee nin mtu alijitoa na kurudi CCM? Toka mwanzo tulijua CCJ wametumwa kutibua kama vilivyo vyama vingi vya upinzani!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 19, 2011

    Naomba msaada, hivi Kada katika Chama cha Siasa ni mwanachama mwenye sifa zipi?
    Je mtu yeyote anaweza kuwa Kada katika Chama chochote?, Inachukua muda muda gani kabla hujawa Kada iwapo si kila mwanachama ni Kada?
    Nisaidieni ili nimwelewe Bw. Kiyabo kwani sikuwahi kujua kuwa yeye ni Kada wa CCM!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 19, 2011

    hodi hodi,tena kwa upendo.wewe ndugu kiabo naomba unitafute nitapoteza muda wangu kukuelezea demokrasia ilipoanzia mpaka ilipo sasa.tena nitaanzia ya magna carta(kwa sasa naomba u google hii)itakusaidia kuoanisha ya leo na demokrasia.(usisahau elements za rule of law,soma kiundani hii pia)sasa kama wewe ni mwanasiasa wa dunia ya demokrasia yawaje hata hujui demokrasia ipo wapi au imevunjwa wapi inanikatisha tamaa nikioanisha na ya sasa ya nchi za mashariki ya kati.mimi ni kijana,ila ni msomi(SHERIA).Najutia usomi,kwani unaninyima raha.Kwakua imeonesha huna ufahamu wa demokrasia,sidhani kama unasifa yoyote ya kuzungumzia demokrasia kwenye maelezo haya kwa JAMII.Mfano Pale ARUSHA,kura za madiwani za kumchagua meya.mtachaguaje meya kama wapiga kura(wachaguaji)hawapo.la hajabu ni pale utawala unapodharua wanachi waliowachagua madiwani wa chadema na mbunge wao.tena ni wengi kwakua mbunge kashinda(mwe)wanasheria wooooote wanajua tayari motokeo ni batili.sijapata marekebisho ya sheria ya uchaguzi,ila najua haiwezekani sheria hii ikapingana na katibu to the extreme.tunataka siku tukimchagua kiongozi,tumpime ufahamu wake wa dunia na tatizo moja baada ya lingine KINDANI,KIUFUNDI NA KISOMI.niuchungu TU,ndio umenifanya nitoke nje ya mada juu ya ccj.Ni uchungu wa kumuona ndugu richard akiwa mbele wakati tayari nimeshaona tatizo lake.ni tatizo kubwa,kwakua dunia ya leo it is too late to fool these people.nakumbuka enzi zile tunaambiwa spinks akipiga anafungwa mkono mmoja,dunia ya leo nenda youtube hapo andika michael spinks utakuta anatandikwa na tyson 1988(nasamehe).Dunia ya leo ni ya ujuaji,sasa huyu ndugu anapotaka kunirudisha wakati sukari kupanga foleni jumatano wanja wa ccm SITAKI KABISAAA.nchi haina amani inautulivu tuu.soma emanuel kant on peace and democrasy~When man is unable to realize his true humanity within the concinnity of reason and the divine ground, explicated within the meta-narrative, his being experiences “a disturbance of noetically ordered existence.”ndugu zangu ingalikua natumia karatasi,basi nikulowa tu kwa karatasi ndio kungenizuia kuendelea.NYERERE ALISEMA 1999 HUKO MBELE NI KUGUMU SANA,SASA NDUGU YANGU ANAPAONGEZEA UGUMU.AHSANTE NA MUNGU AWABARIKI!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2011

    Binafsi sijaona wala sijasikia mahali ambapo CHADEMA wameanzisha vurugu. Huu uongo unaorudiwa mara kwa mara ili uwe kweli hautafanikiwa kutokana na sababu kuwa hali halisi ilivyo kwa wananchi haisaidii uongo uwe kweli. Kila siku mambo yanayoelezwa na CDM hudhihirika kuwa kweli. Na ukweli wa CDM utakuwa umezoeleka kwa wananchi na kuchukuliwa nao kama kitu cha kawaida.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 19, 2011

    Uongo siku zote hutengwa na ukweli! Tulikuwa tunajua wana ccm wote waliokuwa na harakati za kuanzishwa kwa CCJ na aliowataja Mpendazoe ni wote waliohusika.

    Kuhamia kwake Ccm kwa njaa zake ndio kunamfanya leo anakuwa mnanafiki wa dhmaira yake hata kuwa tayari kuongea uongo ambao kamwe hautasafisha ukweli mabo kila siku unazidi kudhihiri.

    SITA na wenzake ndio waanzilishi wa CCJ

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 19, 2011

    Huyu kiabo alijiunga na vyama vitatu ndani ya mwezi mmoja je yeye ni mkweli?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 19, 2011

    Jamaa kafulia sasa kuamua kutoka ndio karudi kwa maharamia wenzake huko CCM..hivi kwanini wanachojua hawa SISIEMU ni kupandikiza chuki kwa raia eti CHADEMA inataka fujo na kwanini sio Chama kilichopo madarakani kwa kushindwa kututimizia matakwa sisi raia wake?
    Hali halisi inaonekana hata bila kuambiwa maisha ya Mtanzania halisi ni bora siku imepita. Wao wanaoingia mikataba feki ndio wananeemeka.. Huyo Kinabo hata usitake kutupandisha hasira za Tarime..

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 19, 2011

    Hongera sana kiabo kwa kusema ukweli. Ni wazi kuwa Chadema wanawafanya Watanzania kama hatuna akili. sisi tunajua mbivu na mbichi. we waache waendelee kupiga kelele lakini kiama chao siku ya uchaguzi. kila siku kelele za kuleta vurugu na maneno ya kizushi na unafiki. kama hawana sera ni heri wakakaa kimya.
    CHADEMA IMEKULA KWENUUUUUUUUUUU!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 19, 2011

    Richard kiabo, you snitch! i hate people like you!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 19, 2011

    siku zote wapenzi wa chadema huamini ya viongozi wao tu na maoni yao ndio sahihi. Hawapendi wengine watoe maoni tofauti na wao wanavyoamini.msionte kuchaguliwa kuongoza nchi hii, mna dalili tosha za udicteta.Hivi lini CCJ au wanzilishi wao kuwa ndio sera ya chama makini kama chadema? mbona wanasiasa wengi wanahama toka chama kimoja hadi kingine? na hata mwalimu alitishia kuhama ccm je nao ulikuwa usaliti. acheni hizi , hubirini sera za chama si kuchambua watu binafsi hamtofika popote kwa kashfa, uongo na kejeli.Ndio maana watu wenye mtazamo tofauti nanyi wanawaona ni wakabila na wadini, maana kila kitu mnakosoa hata kizuri ilimradi kimefanywa na mtu mwenye mtazamo tofauti nanyi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...