
Asalaam Alaykum Ankal
Hebu wawekee hususan vijana wa zamani picha hizi za kina Manara, wachezaji mahiri wa zamani ambao walijulikana sana kwa umahiri wao. Huyo juu kwa jina la kiuchezaji " computer ' .Bila shaka wawafahamu.
Maalim Mrisho

Sunday Manara 'Computer' akikata mbuga

Kitwana Manara 'Popat' akisambaratisha difensi

Kassim Manara akifanya vitu vyake..


kaka issa mie nikisikia haya majina kiukweli roho inauma sana maana zilikuwa hazina allah ametupa tz. sasa leo angala maisha yao hailingani na wao walivyokua, ndio maana nasema roho inaniuma. leo hii angalia tu wanaobahatisha wako wengi tu! ama kweli mabadliko ya dunia ndio yanawabeba watu sasa, hususan mpira wa ulaya. inshort bado sijaona!! siku yupo sunday,kitwn,kassim uwanjan!? ed kibao makazin.
ReplyDeleteila kidogo unaweza kufata majina ya wachezaji kwenye family moja wakawepo! wapo hatukatai ila kwa manara family tofauti ndio nasema hizi hazina zilikuwa!
mdau jp.
wapo wapi siku hizi hao kina manara? Pia Yahya Tostao yupo wapi?
ReplyDeletemichuzi asanre sana kwa hizi picha. hii ni history ya tanzania. kuna yeyote anajua hawa wachezaji wako wapi. wachezaji wengine ni wale wa timu ya tpc arusha chini, watu kama akina hemed seif, sharif, mbwana bushir, john limo n.k. hao walikua mashuhuri sana miaka ya zamani. tanga ilikuwa mbele sana kwenye soccer enzi zao. i hope kuna mahali hizi kumbukumbu zimewekwa.
ReplyDeleteHuyo hapo kwenye picha ya chini mwisho mwenye mpira katikati ni Marehemu Said Mwamba. Hata yeye alikuwa ni kipenzi chetu sana hasa sisi wanaYanga. Tutamkumbuka sana.
ReplyDeleteAnonymous wa 02:30:00 pm huyo sio said mwamba , huyo ni Kassim Manara,na hapo ni uwanja wa karume enzi hizo angalia black september walivyojaa ukutani hawa walijulikana enzi hizo kwa kuvamia uwanjani na kuingia bila malipo.Kassim manara alienda kucheze mpira Austria na kina George (best) Kulagwa, Nico Njohole.
ReplyDeleteNakumbuka fainali ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki kule mombasa kati ya Young Africans na Luo Union ya Kenya hawa jamaa walimweka mtu mmoja kazi yake ilikuwa kumkaba Suday Manara (Computer),kwani huyu jamaa alikuwa anasumbua sana enzi hizo na pia aliwahi kucheza mpira wa kulipwa Ulaya.
ReplyDeleteWewe anony ubayesema Said Mwamba sijakuelewa vizuri.Said Mwamba mimi binafsi nilianza kumsikia yanga mwaka 1986 kijijini kwetu kwenye Kipindi cha michezo cha RTD akiwa ametokea Tabora nadhani ..Hizi Picha za akina Manara sina uhakika kama Said Mwamba(R.I.P) alishaanza 'kukipiga'nadhani ni 'older than' 1985(Sina uhakika sana).Nikiwa Form I 1986 mkoa fulani nilifanikiwa kuwaona wachezaji wa timu za Yanga(namkumbuka beki Yusuph Bana,Charles Boniface,Omar Hussein,Mziba,makumbi,mkambi etc)Tukuyu Stars nilivutiwa na Peter Mwakibibi,Patrick Lumumba,Steve Mussa,Karabi Nrisho?etc.Simba nakumbuka sana Ramadhan Lenny na jibaba fulani nene Zuberi Magoha.Nyota nyekundu nawakumbuka akina Mbarak Mohamed,Mohamed Nyauba,Chibichi,Hamis Dilunga,Ayoub Mzee,Roster Ndunguru,Pazi Ali,Moris Nyuchi,Faustin Kibingwa ha ha ha ha(Kicheko cha Shetani)
ReplyDeleteDavid V.
Wakati huu ulikuwa mzuri na kulikuwepo na maemdeleo ya soka Tanzania,pia hakukuwepo na ujinga wa kuiga timu za Ulaya kama ilivyo sasa,Wachezaji hawakupoteza muda kufanya upuuzi huu,Tujitahidi sana kuacha kabisa ku promoti timu na majina ya Ulaya badala ya kufikiria namna ya kuendeleza soka letu kama ilivyokuwa zamani.Bado tunawakumbuka na tutawakumbuka hawa akina Sunday Manara na wenzie wote.
ReplyDeleteKuna beki mmoja wa simba alisababisha matatizo sana kwa watoto kuumia kwa staili yake ya chogo chemba jina lake aliitwa Omary Chogo (MLUYA)
ReplyDeletehi wananchi tanzanians
ReplyDeletekama mimi na kumbuka the last photo showing kassim manara is from nyamagana stadium but any way i was present in nyamagana stadium on 10th august 1974 when simba lost 2-1 to yanga b being a shabiki of yanga that till now stands a memorial day kuona heroes like sunday manara and sembuli do the footwork for ushindi wa karne