Meneja wa benki ya NMB kanda ya kaskazini, Vick Bishubo (katikati) akifungua mafunzo ya siku moja kwa wajasiriamali ambao ni wanachama wa klabu ya wafanyabaishara wa NMB mkoa wa Arusha.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali yanayoendeshwa na benki ya NMB wakifuatilia kwa makini katika hoteli ya Goldeni Rose mjini Arusha.

Moses Mashalla,Arusha

BENKI ya NMB kanda ya kaskazini imeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wateja wake hususani wanachama wa klabu ya biashara ya NMB, ikiwa lengo ni kuhakikisha mikopo wanayochukua wanamudu kuirejesha pasipo kupata hasara.

Akifungua mafunzo hayo ya siku moja kwa wanachama wa klabu ya biashara(Bisiness Clabu)wa mjini Arusha,Meneja wa NMB Kanda ya kaskazini ,Vick Bishubo alisema kuwa mafunzo hayo ambayo ni ya pili kufanyika mjini hapa,yanalenga kuwaimarisha kibiashara wajasiriamali wanaochukua mikopo katika benki hiyo ili kuweza kumudu kuirejesha .

Bishubo alisema kwamba hatua ya Benki ya NMB kutoa mafunzo kwa wajasiriamali hao ambao wanaochukua mikopo katika benki hiyo ,ni kuwajengea uwezo wa kumudu changamoto zinazowakabili kibiashara sanjari na kukabiliana ushindani wa kibishara.

Alisema mafunzo hayo yamewasaidia pia kuongeza ufanisi katika biashara zao na kutambua gharama za kuendesha biashara,kupanga bei ,kujua masoko na faida inayopatikana katika biashara wanazozifanya.

Hata hivyo, Bishubo aliwatahadhalisha wateja wa NMB hasa wanaochukua mikopo katika benki hiyo kuitumia mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa na kuacha kujiingiza kwenye matumizi mengine yasiyoyalazima ,kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia kuyumba kibishara na hatimaye kushindwa kurejesha mikopo .

Aidha kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo,Malikia Lang’adare kutoka kijiji cha Milongoine alisema kuwa, mafunzo hayo yamemsaidia sana katika kuimarika biashara , kwani kabla ya kuhamasika kuchukua mkopo NMB , alikuwa akiuza chakula kama mama ntilie,lakini baada ya kuanza kuchukua mkopo wa riba nafuu , ameweza kununua ,nyumba ya kuishi ,gari na kufungua duka kubwa la vinywaji mbalimbali vya jumla katika kijiji hicho .

Ametoa ushauri kwa wafanyabaishara wadogo kutoogopa kuchukua mikopo ,kwani Benki ya NMB mbali na kutoa mikopo kwa bei nafuu inekuwa ikiwasaidia kuiendeleza mikopo hiyo kwa kutoa mafunzo kwa wateja wanaokopa na kuwataka wajiunge kwenye klabu ya biashara ya NMB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...