
Mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kukanusha tuhuma za kumiliki mali zinazodaiwa kuzushwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Demokratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila. Ridhwan ametoa siku saba kwa wanasiasa hao kuthibitisha tuhuma hizo vinginevyo amesema atawashtaki mahakamani kwa kumkashifu. Picha na Richard Mwaikenda.
Mafisadi wa awali walimtishia kumburuza Slaa mahakamani lakini mbona hakuna hata mmoja aliyethubutu kufanya hivyo na badala yake wenyewe waliburuzwa mahakamani.
ReplyDeleteRIZWANI MDOGO WANGU MIMI KAMA MIMI SIKUONA SABABU YEYOTE WEWE KWENDA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA TUHUMA HIZO DHIDI YAKO.
ReplyDeleteKUWEKA WAZI TUHUMA HIZO KAMA UNGEITWA RASMI KUTOA MAELEZO KWA TUME HUSIKA DHIDI YA MADAI HAYO.
MDOGO WANGU KUWA MTOTO WA RAISI KIJANA MWENZETU NI DHAMANA KUBWA SANA UTULIVU USHAURI MWEMA NDIO KIOO CHETU SISI WATOTO WA KULIMA KWAKO.
KUZUNGUMZA MAGAZETINI KWENYE TV NA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI NA HATA KWENYE MAJUKWAA YA SIASA NI MUHIMU SANA KUEPUKA IFANYIKE HIVYO PALE AMBAPO KWELI INAHITAJIKA NA UWE UMEOMBWA KWA NA WATAKAOKUMBA WAWE WAMEZINGATIA HESHMA ZOTE NA KUDHMAINI UTU NA UTANZANIA WAKO KATIKA JAMII NZIMA INAYOKUZUNGUKA .
CHANGAMOTO HIZI ZA KISIASA ZILIZOINGIA NCHINI BAADA YA KIFO CHA MUASISI NA MHIMILI WA TAIFA LETU KWA KWELI LIMEPOROMOA MAADILI SANA KUMEKUWA NA KAULI ZINAZOTOKA KWA WANASIASA WA KIZAZI KIPYA AMBAZO KWA KWELI UKITAFAKARI HAZILETI MAENDELEO KWA TAIFA WALA HAZIIPELEKI NCHI KWENYE SAYANSI NA TECHNOLOGY KUMEKUWA NA KULAUMIANA, KUTUPIANA MANENO YA KASHFA LAKINI WANASAHAU KWAMBA WANANCHI NDIO WANAOMIA LEO HII NCHI KAMA RWANDA IMEPIGA MAENDELEO SANA HAKUNA MWANASIASA HATA MMOJA ANAYESEMA AMETUMA UJUMBE WA VIONGOZI KWENDA KUJIFUNZA WENZETU WANAFANYAJE, HAKUNA MWANASIASA ANAETAKA KUFANYA VISIBILITY STUDY KWA AJILI YA MAENDELEO YA NCHI HII BADALA YAKE IMEKUWA LEO HII HATA KUBORESHA MIUNDO MBINU YA BARABARA ZETU, SHULE ZETU,HOSPITAL ZETU HAKUNA KISA KIKUBWA CHAMA FULANI KIMECHUKUA SEHEMU FULANI WACHA WAKOME JAMANI AIBU SIO YA CHAMA NI YA NCHI NA WAGENI WANAPOKUJA WAKIONDA KAMA KUNA SIFA NZURI HAWAENDI KUSEMA NILIKUWA MKOA WA CHAMA FULANI MIUNDO MBINU YAKO NI BORA HUWA WANASEMA NILIKUWA TANZANIA NIMEFURAHI SANA KUKUTA WAMEPIGA HATUA.
KWA HIYO NDUGU ZANGU ENYI VIONGOZI WA SIASA NA FAMILIA ZA WANASIASA TUJENGE TANZANIA YETU FIKIRIENI KWAMBA IDADI YA WATU INAONGEZEKA JENGENI SHULE ZA MAGOROFA KULINDA AKIBA YA ARDHI NA SIO KUJENGA SHULE KAMA TRENI, JENGENI BARABARA PANA NA KUWA NA GUARANTEE TOKA KWA WAKANDARASI YA MIAKA 10 SIO BARABARA MIEZI 6 MASHIMO,WEKENI LAMI BARABARA ZA NDANI ILI KWENYE NJIA KUU KUSIWE NA MISONGAMANO, FUFUENI NJIA ZA RELI CARGO ZOTE ZISAFIRISHWE KWA RELI ILI BARABARA ZETU ZIWE NA MAISHA MAREFU.
FOLENI YA JIJINI DAR TAFUTENI KIWANJA HEKARI 100 KIMARA OFISI ZOTE ZA SERIKALI ZIJENGWE HUKO ILI KUDIVATE FOLENI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WATU NA MAGARI KATIKATI YA JIJI. FLY OVER TUSUBIRI KIDOGO HILI LA UJENZI WA OFISI ZA SERIKALI TUTAWEZA.
NDUGU ZANGU WANASIASA TUELEKEZE NGUVU ZETU KWENYE MAENDELEO HAYO NGUVU ZA KUFANYA HAYO TUNAZO, AKILI TUNAZO, UWEZO TUNAO,SABABU TUNAZO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA.
MDAU
KIPEPEO TOURS
Ilimradi mkono upate kwenda kinywani.... hao ni wana njaa kali na wivu tu, uraisi wamekosa sasa watatafuta kila kitu kumwangusha kila mtu. kwanza mchungaji na siasa wapi na wapi?? wewe ridhiwani endelea kukataa hata kama una mamilioni kweli na wapeleke mbele ya sheria vile vile nachoona tu ni wanatafuta njia za kuwa kwenye habari tu.
ReplyDeleteHuku marekani tunasema "wa sue"
Sijui huyo Slaa, lakini huyo mtikila, mahakamani ndo nyumbani kwake! Kesi Lukuki, lakini hatujawahi kusikia kashindwa au kashinda, ili muradi kesi!
ReplyDeleteKitendo cha kuwapeleka mahakamani kitatuhakikishia unafiki wao. Ukishindwa kuwapeleka, pia itatuhakikishia wasemayo ni kweli!
Ndg. Ridhiwani.
ReplyDeleteMjumbe Baraza la UVCCM(T)
Binafsi nimekua natafuta fursa ya kukuliza ana kwa ana juu ya tuhuma hizi lakini sikupata wasaa, matokeo yake nimekua najiuliza maswali mengi bila majibu....mawili kati yake ni haya:
1.Binafsi yako, toka nimekufahamu, hukuwahi kuonyesha dalili au mtaguso wa fikra za ufisadi na umekua unazungumza namna gani ya kuongeza mawazo mapya ya kumkomboa Mtanzania toka ktk umaskini..Je leo imekuaje utuhumiwe kukumbatia tamaa ya kujilimbikizia mali na hamasa ya kuishi kifahari miongono mwa watanzania maskini?
2.Baba yako ni mkuu wa nchi na kiongozi wa chama tawala ambaye kwa ubinafsi na mapenzi wake hababaishwi, hatetemeshwi na haadhibishi moyo na fikra zake ili ajilimbikizie mali na au hazina kwa namna iwayo yote ili kumstiri sasa au baada ya maisha ya umma na uongozi kukoma kwa kiapo na mkataba kwa wananchi. Je wewe mwanae mpendwa wake ingekuwaje leo ubadilike ghafla na kuwa MUASI(mwasi),mghilibu na chanzo cha kukaribisha mawazo na fikra za ufisadi ktk familia ambayo kabla na wakati huu wa uongozi wa taifa bado WANANCHI WANA IMANI NAYO?
3.Ndg. Ridhiwani, wapo viongozi/watendaji wengi hapa Tanzania ambao mioyo yao inaugua kimya kwa dhihaka ya TUHUMA ambazo si za kweli, zimefinyangwa na zimesemwa na msanii mmoja bila kufikiri au mlevi tu ili kufurahisha jopo/alahiki aliyopo, lakini zikaenea kama moto wa nyikani na kuathiri fikra za wengi ambao hawana nafasi ya kuchambua "kashfa" hizo. Athari hizi zimewakumba na kuwakwamisha watu safi hata ndani ya serikali na chama. Wewe kama mwanasheria umepata bahati ya kipekee ambayo wengi wamekosa. WATUHUMU WAKO WAMEJIANIKA HADHARANI, Kwa Majina na Kauli zao za kuchafua.
VIJANA WENZAKO TULIKOSA MAJIBU. LEO UMEANZA HATUA YA KWANZA YA KUSAFISHA JINA NA KADA YAKO. WATUHUMIWA NI WASANII SANA, TUMIA NGUZO NA MIMBARI YA KISHERIA KWA KIASI CHOCHOTE KITAKACHO KUGHARIMU KWANI HUKUMU YA WAZI IPO KWA KIZAZI(VIJANA) CHAKO.
MAINA OWINO.
kwani Ridhwan akiwa Bilionea kuna tatizo gani?Kuna watoto wadogo kuliko yeye wana pesa na sioni sababu ya yeye kutokua na pesa yeye ni kijana ana nguvu ya kufanya kazi na shule kasoma na si vibaya akitumia nafasi mzee wake aliyonayo kupata pesa bila kufanya biashara haramu.Hata mimi ningepewa nafasi kama yake ningetafuta pesa kwa njia yoyote.
ReplyDeletesasa mlitaka mtoto wa raisi awe muuza madumu ya maji barabarani ndio mjisikie vizuri.
ReplyDeletehii nchi toka CHADEMA wamekuwa na nguvu kiasiasa imejaa umbea na fitina sana. Ujana na fedha zinahusiana nini? Mbona Ndesamburo anapesa toka akiwa kijana hatumuulizi? Mbona Mbowe anapesa hatumuulizi hata kama alirithi kwa babake, (najua hajarithi). Mbona matajiri vijana ni wengi ambao si wanasiasa? Ama kweli SIASA ni jalala lazima ukiingia ukubali kuanikwa utupu... Pole Ridhiwani mwisho leo usiwajibu tena usije patwa na mvi bure kushughulikia fitina.
ReplyDeleteANGALIA KABLA YA KWENDA MAHAKAMANI JIULIZE JE MAHAKAMA WAKIKUULIZA UTHIBITISHE KAMA WEWE SIO BILIONEA UTAWEZA? MANAKE WALE WALIOTAJWA KWENYE LIST OF SHAME WALIUTANGAZIA UMMA KUWA WATAENDA MAHAKAMANI MWINGINE AKASEMA ATAMWOMBEA KWA MUNGU AMSAMEHE LAKINI HAKUNA HATA MMOJA ALIYETHUBUTU KWENDA MAHAKAMANI WALA HUYO ALIYESEMA ATAMWOMBEA KWA MUNGU SIJUI KAMA ALIFANYA HIVYO NAKUOMBA CHONDECHONDE USIENDE MAHAKAMANI MANAKE YANAWEZA YAKAFUMUKA MAKUBWA MPAKA UKAONA DUNIA NI CHUNGU NI SI MAHALA SALAMA PA KUISHI
ReplyDeleteRidhawani hii ndo kukomazwa kisiasa na kufanywa kujulikana zaidi. Kama tuhuma ni za uongo na unajua hivyo wala hauna haja ya kuwapeleka hawa jamaa mahakamani wacha wapige debe kisha yataisha. Hapa mzee ni unapata free promotion and advertisement. Kwahiyo usijali they are making you strong and popular. Who new about Ridhawani bifore! Ni vizuri kuwa kwenye media sometimes ndo kujulikana huko. Kwa jina lako kutajwa na wana siasa inamaanisha wewe ni tishio kwao!
ReplyDeleteMdau hapa nje ya nchi
Hiyo ni kuwaka tu haswa ukweli ukiwa umedhihiri ..bytheway kijana RIDHIWAN unatakiwa uwe mpole kwa usawa huu,kwani hayo mabilion ya shilingi ni vile vile ni ulaji unaopata kupitia we sasa ni line kuweza kuwaunganisha watu wenye mali au wafanyabiashara kumuona babako au sehem mhim za kufaidika kwao ,au kuweza kuwekeza bila ya mlolongo na kupata difence kutoka kwa mheshimiwa rais ,we unaenda kama midle man sidhan kama kuna kosa ww kuweza kuwa na pesa na watu wenyewe kwa sasa wanakutafuta wakupe pesa ili wawe karibu na ww ili waweze muona babako,mheshimiwa rais,inthe mean time haina haja kuwaka we komaa nao na endeleza maisha yako ya future kwa baadae we na familia yako nchi au ndani ya nchi na uwekeze kupitia mfumo wa maisha yanavoenda kwa kasi,hio sioni sababu ya kumtuhum kuwa KIJANA RIDHIWAN ANA MABILIONS,hizo shinlingi ni jitihada zake kuweza kuishi na kukomaa kama ni utafutaji,na vile vile mjue yeye ni mndendaji wa kazi anaejituma kwa nguvu zake na amekaa shule vile vile ,kitengo alichokuwa au anachokifanyia kazi ni ulaji ,kwani kuna case ,kuna mikataba inahitaji mawakili,si yeye tu wengi tu mawakili wako safi mbaya mno kimaisha kwani ni kitengo binafsi kupata offer nyingi na kuwa na pesa za kuwajibika ,anyway komaa na usitetereke ,almhim Omba sana mungu uwe katika ulaji huo huo ,advices yangu jiepushe na siasa,ufanye kazi zako vizuri kuwa mwanachama tu wa CCM kwani ndio kipendacho roho.Mdau BAGAMOYO
ReplyDeletemie maoni yangu ni kwamba kijana ajifunze kuongea bila kurusha mikono...kwani tunategemea awe mfano kwa vijana wenziwe..ukirusha rusha mikono unaonekana una jazba na jazba humilikiwa na wasioona mbele....
ReplyDeleteJamani siasa ni mbaya sana, mkumbuke hata Mwl Nyerere alikuwa anaambiwa anamapesa uswiss na nchi za nje, walikuwa wakisema wakati watanzania hawaruhusiwei TV yeye kwake zilikuweko, dollar kupata kwa kibali watoto wake wanizichezea vitu ambavyo vilikuwa uongo mtupu, mpaka alipokufa ndio wakajua ni kweli hakuwa na vitu hivyo. Hilo moja, halafu huyo Slaa yeye anasema anataka kuondoa umasikini mtu akiwa tajiri yeye anakasirika, inaonyesha undumila kuwili wake. Mbona Mbowe ana-mihela hasemi, kamchukua mke wa mtu kwa pesa kamghilibu yule bwana mume wa watu kwa pesa, yuko kimya....! Dunia imekwisha hata mchungaji anasema uongo?
ReplyDeleteHehhehhehhheee! Lol! Wacha nicheke ninenepe mswahili mie nikonde nna mume? Labda Kaka Issa hapa anioe mke wa watatu! Tena nacheka kama mazuri vile, kumbe nchi hii ni watu wa kutoka upande fulani tu ndio wanatakiwa wawe na hela? Au watu wa aina fulani tu ndio wanatakiwa wawe na hela wengine wote wakiwa na pesa basi ni mafisadi ila wao wakiwa na pesa ni haki yao!
ReplyDeleteAu kwa kuwa zamani zile yule Mzee wao alikuwa anaweka signature yake kwenye pesa basi pesa zote mali zao wengine wote ni wezi? Mbona mwaleta hadithi ya wamasai na ng'ombe? Maana mmasai anadai ng'ombe wote ni mali yake na atakapomkuta popote basi kaibiwa yeye na anahaki ya kumrudisha kundini. Huyo Mtikila ana pesa chafu na dhulumati fisadi mkubwa na huyo mwenzie ndio hata hatusemi maana yeye sasa ni bilionea kila siku yu akula pesa za watu kutoka nje. Haya na hao kina Mbowe na Ndesamburo wao pesa zao ni halali? Wanalipa kodi ipasavyo TRA bila kukwepa, hawana biashara za haramu zilizojificha migongoni mwa biashara halali? Hebu nifunge kalomo kangu kwa biashara halali Bongo kamwe huwezi kuwa tajiri bilionea kama hao wenye kuona kuwa na pesa ni haki yao.
Waache waseme mchana usiku watalala na hivyo mnavyokaa kuwajibu jibu ndio mnawapa kichwa, mnachotakiwa kufanya sio kujibu bali kufunua madudu yao kisha kuyatangaza hadharani kama jamaa alivyomnyamazisha Mtikila kwa kumtolea siri zake za kwenda kuomba pesa kwake. Mnamsikia siku hizi anamfuata fuata kwa maneno yule mdosi tena? Kakoma mwenyewe!
Ridwhani mimi sikufahamu wala huniafahamu:Najua utasoma hapa na baba yako atasoma..Kwanza nakupa pole sana najua inavyouma mtu akikupakazia uwongo yaani kuna kitu huwa hadi kinang'ang'ania kooni lakini ukishamweleza rafiki yako huwa kinaachia..sasa umeongea na waandishi wa habari nadhani ile jazba uliyokuwa nayo imepungua.
ReplyDeleteUshauri mwingi humu umeambiwa usiende mahakamani..na mimi ni mmoja wa hao..jaribu ku-'control temper' yako fanya shughuli zako kama kawaida..sisi binadamu ni watu wa kusahau baada ya muda watu watasahau na wewe utasahau...Mimi nilishau kama ulisemwa ingawa nilisoma..mahali lakini leo wewe ndiye umenifanya nikakumbuka(huo ni mfano mdogo)..Mzee Jk mwambie kijana atulie ndiyo ukubwa huo..ndiyo anakua hivyo.
David Villa
nyie wabongo kwanini mnapenda kuwatetea waalifu nyie?? kijana kuwa na pesa siyo tatizo, tatizo je pesa hizo ulizipataje? majibu yake kuwa eti magari ya bei mbaya anayoendesha huwa anaazima kwa watu nyie mnayaona yana akili ndani yake?? toka amalize shule hana ajira yoyote ya maana inayofahamika inayomwingizia pesa kama mimi na wewe na pia pamoja kuwa yeye ni mwanasheria lakini hajawahi kuonekana hata siku moja mahakamani akitetea watu. acheni hizo wabongo.
ReplyDeleteEEeeeeh, eeeeeeeeh ingekuwa ni mimi ningecheka kama baba yako, piga makofi kushangilia maana sijatukanwa na kama huna kweli ni baraka hizo wanakuombea, kwani we unakasirika nini ukiitwa tajiri au hujazipata kwa halali, Bwana mdogo kila mtu anasema kutokana na alivyo, kesho nenda msikitini sali upate hela pia shukuru kuwa haujatuhumiwa kuuza unga.Nadhani wanyamazao wanajua mengi kuliko wasemao. Fanya zoezi kama mtoto wa mtu mkubwa ili tukukumbuke kesho. Wala usipoteze muda, hela na nguvu kupigana na hewa.
ReplyDeleteMdau - UK west
Naona wachangiaji wengi hapo juu wamwonea huruma RIdhiwan!! Mi ninafurahi kwa tamko alilolitoa kwamba anataka Mheshiwa Silaa na Mchungaji watoa vielelezo!! Ni hoja hatua yenye kuonyesha kukua kisiasa. However waliomtuhumu Ridhiwan, ni watu wenye kuheshimika haswa Mheshimiwa siliaa!! Aliibua scandal nyingi na zilidhibtika na watu kuwajibika!! Hivyo mi nawashauri watanzania wenzangu kuto kuwa na jaziba na kusubiri hatima ya hili pia..
ReplyDeleteTujifunze kueheshimu na kutambua nafasi ya upizani katika tawala za kileo.
Ridhiwani mimi binafsi sikukusikiliza, nilikuwa napita sehemu nikakuta wamefungulia televisheni nje nikakuona ukiongea nikajua kuwa ndo umeanza kudefend ishu yako, maoni yaliyotolewa hapa ni ya busara yafanyie kazi, sina uhakika kama ulifanya hili, nafikiri ingekuwa vizuri kama ungetaja mali unazomiliki kwa sasa na kutaja vyanzo vya mapato pia. Suala la kuwapeleka mahakamani hawa waheshmiwa nafikiri wewe ndo unaujua ukweli, kama unaona umesingiziwa bora uende mahakamani, ila kama unaona hakuna ukweli we nenda tu mahakamani itsaidia kuwa fundisho kwa hao wenye kusingizia wenzao.
ReplyDeleteNkyabo- Bongo
Mimi nafikiri Ridhiwani ana haki ya kumiliki pesa kwa sababu, kwanza yeye ni mwanasheria na amewahi kuzifanyia kazi kampuni za Deep Green Finance na Imma Advocates na kwa sababu ni kampuni zenye kulipa vizuri basi sitashangaa kusikia kwamba ana pesa. Pili yeye si yuko kwenye yuvisisemu na kule anapata mshahara, basi nafikiri ni vema akawapeleka mahakamani hawa waliomchafua.
ReplyDeleteHivi Ridhiwani anamiliki mali gani jamani!!! Mbona tunamuona kwenye magari yetu ya usidi na tunakula naye kwenye maeneo ya kawaida tu. Nina wacwac hata nyumba nayokaa ni ya kupanga bado hajajenga.
ReplyDeleteyeye aende mahakamani ukweli ufahamike,kusingiziwa kunaumiza taswira mbele ya jamii
ReplyDeletendugu zangu hivi kwa mawazo yetu mafupi je tungetarajia Ridhione akubali kuwa yeye kweli ni Bilionea? au ndo karukiwa na magamba
ReplyDeleteBongo tambarare!!! kaazi kweli kweli
ReplyDelete