Pichani kulia na kushoto (Rolland Barnabas na Francisco Nyambo) wakishangilia ushindi wao wa kuingia kwenye msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti fiesta freestyle 2011,ndani ya Lips Club,Isamilo jijini Mwanza.Washiriki hawa watajiunga na wenzao kutoka mikoa mingine na kutinga ndani ya jiji la Dar kutimiza kile kilele cha msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta 2011,hapo baadaye.
Majaji wakionekana kuduwaa kimtindo mara baada ya ukumbi kulipukwa na mayowe,wakati wa kumtaja mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti fiesta freestyle 2011,ndani kiota cha maraha cha Lips Club,Isamilo jijini Mwanza jioni ya leo.
Washabiki kadhaa walijitokeza kuwapngeza wenzao mara baada ya kutajwa kuwa wote wawili,yaani Rolland Barnabas na Francisco Nyambo ndio waliofanikiwa kunyakuwa ushindi mnono wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011 kati ya washiriki wapato 40.
Ulifika wakati wa kumtangaza mshindi wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta freestlye 2011,Pichani shoto ni Mratibu Mkuu wa shindano hilo Fatma Hassan a.k.a Dj Fetty akizungumza jambo kabla ya kumtaja mshindi jioni ya leo ndani ya Lips Club,Isamilo jijini Mwanza,anaefuata ni mshiriki aliyeingia fainali aitwaye Rolland Barnabas,na mwisho kulia ni mshiriki mwingine aliyeingia fainali aitwaye Francisco Nyambo.
Ilikuwa ni full mzuka kwa washiriki kwani walionesha uwezo na umahiri wao wa kucheza na maneno,huku hadhira ikishangilia kila wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...