Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimshauri Mkuu wa kitengo cha Kemia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Phillip Joseph jinsi gani wanaweza kufanya kazi ya kuchuja maji hadi kufikia hatua ya kuwa maji safi na salama kwa ufasaha zaidi na hivyo kuingia katika soko la ushindani wa biashara. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimsikiliza Sara Rubagumya (wa kwanza kulia) mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Tegeta iliyopo jijini Dar es Salaam kuhusu jinsi ya kuzalisha umeme kwa njia isiyo na gharama. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (watatu kutoka kushoto) akimsikiliza Salim Buyogera mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya Sekondari Mbeta iliyopo jijini Mbeya alivyokuwa anaelezea jinsi vipande vya mabati vinavyoweza kuhifadhiwa na kutumika kufanya mambo mengine wakati wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Kushoto kwa waziri ni Naibu waziri wa wizara hiyo Philipo Mulugo na kulia kwa waziri ni Chande Othman mwenyekiti wa chama cha wakemia nchini.
Elizabeth Mlay (kulia kwa waziri ) mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi ya kutengeneza dawa ya kusafishia na kuondoa harufu chooni. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...