Waziri wa Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali hawapo pichani, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya shirika la simu nchini TTCL iliyozinduliwa leo katika makao makuu ya kampuni hiyo jengo la Extelecoms jijini Dar es salaam, Enos Bukuku ndiye mwenyekiti wa bodi hiyo mpya.
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya simu TTCL Said Amir Said akizungumza na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya kampuni hiyo iliyozinduliwa leo jijini Dar es salaam, kulia ni Mwenyekiti mpya wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo na kushoto ni Mwakibinga Mihalale mjumbe wa bodi.
Waziri wa Mawasiliano Makame Mbarawa kulia akimpongeza Enos Bukuku Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TTCL, mara baada ya bodi hiyo kuzinduliwa rasmi katika makao makuu ya kampuni hiyomtaa wa Samora jijini Dar es salaam leo, katikati ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Said Amir Said.
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya simu TTCL Said Amir Said akizungumza na wageni waalikwa katikati ni mjumbe wa bodi Mwakibinga Mihalale na kushoto ni Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa bodi hiyo Jaji Joseph Warioba.
Wakuu wa vitengo mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo kutoka mkulia ni Kazaura Kamugisha Mkurugenzi wa ufundi, Ernest Nangi Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko na mwisho ni Mkurugenzi wa idara ya fedha Shaban Mrisho.
Waziri wa Mawasiliano Makame Mbarawa katikati akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa shirika la TTCL, wajumbe wa bodi pamoja na wakurugenzi wa vitengo mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...