Picha ya Marehemu Tulakela Samnyuha, mama mzazi wa Mbunge wa Njombe Kusini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Anne Makinda , aliyefariki dunia ghafla tarehe 5/5/2011 mjini Dodoma.
Jeneza lilibeba mwili wa Bibi Tulakela

. Mhe. Makinda akiwashukuru wana-Dodoma kwa ushirikiano waliompa wakati huu wa kuomboleza msiba wa Mama yake

Mama Anne Makinda akifarijiwa na watumishi wa Ofisi ya Bunge
. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Nsekela (kulia ) na Mhe. Deo K. Sanga Mbunge wa Jimbo la Njombe Kaskazini (kushoto) Wakimsindikiza Spika Makinda (katikati) kwenye ndege iliyobebe mwili wa marehemu mama yake tayari kwenda mkoa wa Njombe kwa ajili ya Mazishi

Spika Anne Makinda (kulia) akiwa na dada yake wakati wa Ibada mjini Dodoma leo.

. Spika Makinda akitoa heshima za mwisho kwa marehemu mama yake akisindikizwa na waheshimiwa Wabunge. Kushoto kwake ni Mhe. Mama Anna Abdala (Mb). Kulia kwake ni Mhe. Bura (Mb) na Mhe. Lediana Mng’ong’o (Mb)
Spika Anne Makinda akisindikizwa baada ya ibada

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2011

    Kwenye picha ya tatu kutoka juu Mh. Makinda amefanana sana na marehemu mama yake .... cheki hata mdomo alivyouweka sawa sawa na picha ya marehemu.

    Pole kwa kufiwa Mh., Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...