Mtaalam wa tiba za asili na tiba mbadala kutoka Mwanza Bw. Musa Chacha akitoa maelezo ya namna dawa zake zinavyofanya kazi kwa mkuu wa wilaya ya Musoma Kepteni Mstaafu Jeofrey Ngatuni (katikati) alipotembelea mabanda ya maonyesho wakati wa Siku ya Utamaduni Duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa mkoani Mara.

Mwalimu wa kikundi cha kutoka Tarime Bw. Gabriel Ngereine (kulia) akiliongoza kundi hilo kutoa burudani kwa wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya Karume manispaa ya Musoma kuadhimisha Siku ya Utamadauni Duniani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Mara.
Mzee Fabiano Rugula mwenye umri wa miaka 97 kutoka katika kikundi cha Jeramoro Rorya akitoa burudani kwa wananchi waliojitokeza kusherehekea siku ya utamaduni Duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Wasanii wa vikundi mbalimbali kutoka mkoani Mara wakiingia katika uwanja wa Karume katika manispaa ya Musoma kuadhimisha siku ya Utamaduni Duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa mkoani Mara.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...