brother michuzi,habari za kazi.
Mimi ni mpenzi sana wa nyimbo na mashairi.Kuna shairi moja lilitamba sana kipindi majeshi ya tanzania yalipomaliza vita vya kagera hapa naongelea miaka ya 79/80.Silikumbuki lote ila nakumbuka vipengere kadhaa tu.
Iddi Amini jasusi tena hili joka kuu,limefanya uvamizi kuteka ardhi yetu
hatuna kazi nyingine lazima tutalipiga,ndipo litakajua Tanzania ni ya watu
Kijiita alhaji eti alihiji Maka,tangu lini Alhaji akachinja mwanadamu
huu wote ni utani anamtania Mungu,japo awe Alhaji sisi tutamkung'uta...
Naomba sana wenye data za shairi hili wanisaidie ili nipate vionjo vya enzi zetu.
MAY GOD BLESS YOU,I LOVE YOU,I LOVE JESUS.
AMEN
Nadhani itabidi tuanzishe shairi lingine la walrushwa na Mafisadi kwani wao kwa sasa ni wabaya kuliko Iddiamini. Enzi za ediamini watoto walikuwa wankwenda shule znazojulikana , dawa zinapatikana, na umeme ulikuwa unapatikana.
ReplyDeletenami naungana na huyu anayetafuta mashairi wa hii wimbo mimi mwenyewe nikuwa naipenda sana tu japo sielewi inapatikana wapi na mimi natakakuongezea na mimi natafuta sana zile nyimbo za maombolezo wakati wa kifo cha mwalimu julias kambarage nyerere hasa zile alizoimba capten comba na bata muzika band naombeni wanaoelewa namna ya kuzipata hizo nyimbo mbarikiwe woote wanaotembelea hapa na kaka michuzi kwa kazi yake nzuri
ReplyDeleteduh! mambo kama haya muulize chemi che mponda atakuwa anayajua.
ReplyDeleteIddi Amini jasusi, joka hili joka kuu,
ReplyDeleteLimefanya uvamizi, kuteka ardhi yetu.
Hatuna kazi nyingine, ila nikulifukuza,
Ndipo litakapojua, Tanzania ni ya watu.
Tukiliita beberu, bure tunalitukuza,
Iddi Amini Bawabu, Makombo yanamuponza,
katumwa na makaburu, kuja kutuangamiza
hatuna jingine jibu, bali nikumkung'uta.
Kwanza tulimdhania yeye ni mwenda wazimu,
Sasa tumembaini kumbe amelewa damu
Kawachinja masikini, tajiri na maimamu,
na maaskofu ndani, wote amewanywa damu.
Nimeshasahau mengine lakini nadhani Radio Tanzania wana huo mkanda. Please tunaomba mweke kwenye CD nyimbo zote za vita vya kagera sababu inatukumbusha mbali. Mimi nilikuwa Korogwe TTC. Tulikatazwa kwenda likizo ila siku tuliporuhusiwa ilibidi nisafiri na lori la mafuta toka Mwanza mpaka Bukoba na tulipofika Karebe nilivuliwa suruari sababu the day before nasikia kuna mwanamke alikuwa na bom kwenye suruari alitaka kulipua daraja la Karebe. We acha tu. halafu kufika nyumbani mizinga ilikuwa inalia usiku kucha. Baba alitugawia pesa kila mtu ili tukikimbia kila mtu awe na at least kianzio cha nauli. Kulikuwa na maandaki ya L waliyaita ya Yelo (nadhani mkufunzi alikuwa mtani hakuweaa kusema L)
na ule wimbo wa Ndugu zetu ndugu zetu, mlio mipakani imarisheni nguvu tuwe imara, ili tuilinde nchi yetu, tuhakikishe hatuchezewi tena na yeyote. Inywe Kyaka,.... Mulio muta ne
MH Dunia ina propaganda sana hii!!! eti idii amini jasusi ! someni historia mjue ukweli kwanza ! mnaweza kujua hao walimwita iddi amini jasusi wao ndio majasusi ! ...
ReplyDelete