Mchezaji wa timu ya mkoa wa Singida, Yahaya Ramadhani akimweka chini mchezaji wa timu ya mkoa wa Ilala, Erick Mawala wakati wa Robofaianali ya kwanza ya Michuano ya KiliTaifa Cup inayofanyika jijini Arusha. Ilala ilishinda 3-0 na kuivua Singida ubingwa.

Wachezaji wa timu ya mkoa wa Ilala wakishangilia goli la pili dhidi ya timu ya mkoa wa Singida wakati wa Robofainali ya kwanza ya michuano ya KiliTaifa inayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Ilala ilishinda 3-0 na kuivua Singida ubingwa.

Wachezaji wa timu ya mkoa wa Singida na Mkoa wa Ilala wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Robofainali ya kwanza ya michuano ya Kili Taifa inayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Ilala ilishinda 3-0 na kuivua Singida ubingwa.

Na Mwandishi Wetu,Arusha

MABINGWA Watetezi wa michuano ya Kili Taifa Cup 2010 timu ya Mkoa Singida (Kidai Shooting) imeaga mashindano hayo kwa kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa timu ya Ilala, katika mchezo uliyofanyika kwenye Uwanja sheikh Amri Abeid.

Dakika ya 12 ya mchezo Salum Mpakala, aliipatia Ilala goli la kwanza baada ya kupiga shuti la mbali lililombabatiza beki wa Singida Charles Msuka na kumalizia mpira huo wavuni.

Mchezaji Vedastu Kaunda, aliipatia Ilala goli la pili baada ya kupata pasi toka Said Ahmed aliichanganya safu ya ulinzi ya Singida n kufunga goli hilo, mpaka Ilala ilitoka kifua mbele kwa mabao 2-0.

Katika kipindi hicho kila timu iliweza kufanya mashambulizi kadhaa lakini safu ya ushambuliaji ya Singida ilionekana kukata tamaa mapema.

Dakika ya 59 Omar Matuta aliipatia Ilala goli la tatu ambalo lilidumu mpaka mpira unamalizika.

Ilala itakutana na mshindi kati ya Arusha na Mwanza waliokuwa wanacheza saa 10.alasiri.

Mashindano ya Kili Taifa Cup yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kili manjaro Premium Lager na masuala ya habari kuratibiwa na Kampuni ya Executive Solution

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...