Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Anne Makinda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mzee Hubert Mbaga
Akitoa salamu za rambirambi katikati msiba huo, Spika Makinda aliwataka watanzania kuienzi amani ya taifa la Tanzania kama alivyofanya marehemu Mbaga wakati wa uhai wake kwani alimfahamu vizuri kwa kufanyakazi naye kwa karibu. Picha ndo ni ya marehemu Hubert Mbaga.
Kutoka kulia Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM) Mhe. Abdulrahman Kinana, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Athuman Mdoe na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Raymond wakiwa miongoni mwa maelfu ya wananchi walioshiriki katika mazishi ya aliyewahi kuwa Mbunge wa Arusha Mjini (1980-1985) marehemu Hubert Mbaga aliyefariki Aprili 27 na kuzikwa jana nyumbni kwake Usangi.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akipanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana ya Mtakatifu Theresia wa Avila iliyoko katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro jana. Hii ni shule ya kwanza ya wasichana katika wilaya hii. Aliyeshikilia mti huo ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Athman Mdoe. Shule iko chini ya usimamizi wa jimbo Katoliki la Same na inaongozwa na Masista wa Shirika la Grail Tanzania. Sekondari hii yenye wanafunzi 316 na waalimu 16 inaongozwa kwa tunu kuu tano za maadili na kujitambua ambazo ni kujibu maswali yafuatayo: Mimi ni nani? Niko wapi? Nimekuja kufanya nini? Kwa nini ninasoma? na Niko na nani? (kwa maana ya marafiki).
Baada ya upandaji wa mti huo, Spika Makinda aliukabidhi kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Veronica Bwana, autunze na wakati huo huo kuzungumza na wazazi wa walezi wa wanafunzi kuhusu umuhimu wa kuwasomesha watoto wa kike na umhuhimu wa kuilinda amani ya Tanzania. Pia aliwataka watanzania wote kushiriki katika mchakato mzima wa kuundwa kwa katiba mpya ya Tanzania.Picha na Prosper Minja-Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2011

    RIP Mzee MbagaWe will dearly miss you!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...