Mkurugenzi wa taasisi ya Chief Promotions,Amon Mkoga (kulia) pamoja na Meneja wa Bia ya Balimi,Edith Bebwa wakionyesha moja ya matangazo ya Tamasha na Mtemi Mirambo.
TAMASHA la ngoma za utamaduni na maonyesho ya biashara la Mtemi Milambo linatarajiwa kurindima kuanzia Julai 8 hadi 10 kwenye Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa taasisi ya Chief Promotions ambao ndio waandaaji,Amon Mkoga, alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuenzi na kuuendeleza utamaduni wa Kitanzania, hususani makabila makubwa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga na Mwanza, ambao ni Wanyamwezi na Wasukuma.
Mkoga alisema pia michezo na maonyesho ya bidhaa zenye asili ya Kitanzania pia vitakuwepo,kama vile mchezo wa bao na kurusha mishale.
Alisema, Ijumaa ya Julai 8 shughuli itaanza saa 4:00 asubuhi hadi 12:00 jioni na kuendelea kwa muda huo huo hadi Jumapili Julai 10.
Mkurugenzi huyo alizitaja baadhi ya ngoma zitakazokuwemo wakati wa tamasha hilo kuwa ni pamoja na Manyanga, Maswezi, Uyeye, Bagalu, Bagika, Bazuba, Radu na nyinginezo.
Naye Meneja wa Bia ya Balimi, ambao ni kati ya wadhamini wa tamasha hilo,Bi Edith Bebwa, alisema wameamua kujitosa kudhamini tamasha hilo kwa mara ya pili ili kuwaenzi wateja wa bia hiyo ambayo ni mahususi kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.
“Ngoma hizi za Wasukuma na Wanyamwezi huchezwa sana wakati wa mavuno, hivyo kwa kuwa Balimi ni bia ya mkulima tumeona tuungane kusherehea pamoja wakati wa mavuno huku tukienzi utamaduni wa Kitanzania,” alisema Bebwa.
Mgeni rasmi katika Tamasha hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Abeid Mwinyimusa.
Kauli mbiu ya Tamasha hili mwaka huu ni KUSHOKE KUKAYA yaani turudi nyumbani tafsiri ya Kiswahili toka kinyamwezi.
Mbali ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi, wadhamini wengine ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ubalozi wa Switzerland ,Kalunde General Supplies, UNESCO na Fly 540(Shirika la ndege),Geita Goldmines, Magic Fm, Channel Ten na TBC.



LAZIMA TUULIZANE BWANA:
ReplyDeleteMjomba Michuzi.(sina uhakika kama ni yule mjomba,ambaye Mshairi Mpoto ataka onana naye au la!).
kuna swala ambalo, kwa mtazamo wangu kuna umuhimu wa kulimulika haswa..iwe kwa kurunzi au Kibatari lakini swala hili tulimulikeni jamani.
siku hizi umezuka mtindo kama si utamaduni mpya wa wasichana au mabinti (hasa wa Vyuo vikuu) na wale ambao wapo maofisini wakiwa bado wana kaharufu ka vitabu na biki,KUSHABIKIA SOKA AU KANDANDA LA MAJUU. Kwa kumbukumbu zangu, mtindo huu ni mpya kabisa wenye umri takribani miaka miwili tu.kila binti skuizi utamsikia ,,OOh sjui mimi Man U, wengine Arsenal, wengine sjuni nini huko " na hapo juzi wakati wa fainali za kombe la ubingwa wa Ulaya ndio ilikuwa balaa mitaani huko na kwenye viringe vya ,,Facebook" swali langu ni JE? HAWA MASHABIKI WAPYA WA ULINGO WA SOKA WAMETOKEA WAPI??? au ndio muendelezo wetu wa kufuata mkumbo ambao sisi tumejizoelea kuwa nao? maana mtindo ukiingia utashambuliwa na watu watatengeeza pesa haraka haraka na miezi michache tu hakuna kitu tena..
mpwao mwenye tabia ya uchokozi
Popobawa:
Asanteni kwa kuendeleza mila yetu mimi ni mnyamwezi asilia (Mgosya wa Mbasa) mzaliwa na elimu yangu hapo hapo mboka nachoomba ni kwa mheshimiwa Bw. ISMAIL RAGE mbunge wetu mimi na yeye ni wazawa hasa na tunaijua Tabora yetu sasa ajitahidi kuleta maendeleo na sisi tupo nae maana mkowa wetu umesahaulika licha ya kuona takribani viongozi wote wa serikali ya tanzania wamesoma tabora au kuwepo kikazi lakini leo wanaacha mji wenye HADHI kubwa uonekane kiasi hicho ila wakati wa kuomba kura zetu mnatupigia magoti. maana ni bora tumkumbuke mkoloni TABORA ulikuwa mji hasa kuliko hii miaka 50 ya uhuru. na hii si tabora tu hebu mikowa yote kanda ya magharibi viongozi wabaguzi wakubwa na aibu hawana.balaa
ReplyDeleteMimi ni mzawa original kabisa pale tabora mwanza road naskitika kuona kwamba viongozi most of them walienda shule Tabora school, Tabora Boys, tabora Town school, pia katika kipindi cha kulilia uhuru nchini kwetu mwalimu alifanikisha sana kwa kupitia mkoa wa tabora na viongozi wote wanajua hata Mr president Jk analijua hilo, na kama jeshi kubwa la usalama ambalo lilisaidia kumtoa Iddi amin Dada wa Uganda lilitoka Tabora Sasa viongozi Mnaosema Mnaiongoza Tabora... hamuoni haibu? wenzenu wote wanajenga mikoa yao except ninyi ''How shame'' You need to think before you ask citizen to vote for you.
ReplyDeleteI was There last month hakuna hospital private except kitete, hakuna barabara zilizopo ni vumbi tupu na mabonde, soko lipo moja, (mnawavunja nguvu wawekezaji katika mkoa huo wanaona ni waste of space) Mji utafikiri umepigwa bomu jamani hebu liangalieni hilo