Afisa mauzo wa TBL mkoa wa Kilimanjaro Edmund Rutaraka(katikati)akimkabidhi kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Meja Jenerali Said Kalembo kiasi cha shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya maandalizi ya timu ya mkoa wa Kilimanjaro.kushoto ni makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro(KRFA) Darabu M.Darabu.

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imekabidhi kiasi cha shilingi milioni 1.5 timu ya mkoa wa Kilimanjaro “Kilimanjaro Warriors kwa kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kili taifa cup.

Fedha hizo zilikabidhiwa jana kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Meja jenerali ,Said Kalembo ambaye pia alikabidhi fedha hizo kwa viongozi wa chama cha soka mkoa KRFA.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo afisa mauzo mkoa wa Kilimanjaro Edmund Rutaraka alisema kampuni hiyo imetoa kiasi hicho cha fedha ikiwa ni sehemu ya udhamini pamoja na kuwapa motisha wachezaji.

“Mh mkuu wa mkoa ,kama lilivyo jina la mashindano lenyewe Kilimanjaro Taifa cup na mkoa wetu ni Kilimanjaro ,tukasema ni vyema tulete pesa hizi ili ziweze kusaidia timu katika maandalizi na wachezaji waweze kupata motisha”alisema Rutaraka.

Alisema kampuni hiyo itaendelea kusaidia maendeleo ya soka ikiwa ni pamoja na kuwapa ari wachezaji ili waweze kushiriki mashindano mbalimbali kwa kiwango cha juu.

Akizungumzia zawadi za mwaka huu Rutaraka.alisema mshindi wa kwanza mwaka huu atapata shilingi milioni 40 ,wa pili miliono 20 wa tatu milioni 10 huku mchezaji bora na mfungaji bora wakiambulia kiasi cha shilingi million 2 kila mmoja.

Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa ,Kalembo aliipongeza TBL kwa jitihada zao na kutoa mwito kwa makampuni mbalimbali, mashirika na watu binafsi kujitokeza kuisaidia timu ya soka ya mkoa wa Kilimanjaro ili iweze kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Kalembo alisema kuandaa michezo kama mashindano ya Kili taifa cup ni gharama kubwa na kutokana na hilo TBL inapaswa kupongezwa kwa hilo na kutoa mwito kwa kampuni nyingine kuiga mfano huo ili kuinua michezo mingine badala ya soka pekee.

Aidha Kalembo alisema kutokana na jina la mashindano hayo,Kilimanjaro taifa cup,linaendana na na jina la mkoa ,mlima Kilimanjaro na bia inayodhamini mashindano hayo ni TBL Kilimanjaro kuipa msaada zaidi timu hiyo ili iweze kupeperusha vyema jina hilo.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro Darabu M Darabu alisema kiasi hicho cha fedha kitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuisadia timu hiyo.

“Kwa sasa timu ina hali mbaya sana ,hali inayopelekea wachezaji kutaka kugoma tunaomba wakazi wa Kilimanjaro kama walivyofanya wakazi wa mikoa mingine waisaidie timu yao iweze kufanya vizuri”alisema Darabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2011

    Katika picha hii kuna mmoja amefanana na Babu wa Loliondo.
    Teh Teh Teh!!!!!!!!!!!!!

    Mkatunist, Mnyanjani - Tanga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...