
Ligi ya Taifa ya kikapu inatarajiwa kuanza tarehe 7 -14 Mei, 2011 katika uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam.Tunatarajia timu bingwa za kila mkoa kushiriki pamoja na mshindi wa pili.
Bingwa mtetezi wanawake na wanaume watapewa nafasi ya kutetea mataji yao Mkoa mwenyeji umepewa nafasi ya kuongeza timu 4 zaidi ili kuleta ushindani na hamasa katika mashindano haya.
Mashindano haya yatashirikisha wanaume na wanawake, wanaume ni kama nilivyoeleza hapo juu na kwa upande wa wanawake timu zote za kikapu toka nchi nzima zimealikwa kushiriki, lengo likiwa ni kuhamasisha zaidi wanawake kushiriki katika mchezo wa kikapu.
Kila timu itasajili wachezaji 12 na viongozi 3 ambao ndio wataruhusiwa kukaa katika benchi la ufundi.
Waamuzi na makamisaa watakachezesha mashindano haya ni na watatauliwa na kamisheni ya Makocha ya TBF na ni wale wanye beji za FIBA, Kanda ya 5 na wa Taifa.
Tuanatarajia mashindano haya yatakuwa na ushindani wa hali ya juu kwa sababu washindi 2 wa juu wa kila jinsia yaani wanaume na wanawake watapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kutafuta Bingwa wa kikapu wa kanda ya 5 yatakayofanyika mwezi wa 8 mwaka huu hapa Dar es Salaam. Pia washindi hao watashiriki kombe la Muungano mwezi Juni, 2011.
Bado timu zina nafasi ya kuthibitisha kushiriki ligi hii hadi sasa, na natumia nafasi hii kutoa wito kwa viongozi wote wa mikoa ya Tanzania Bara kuhakisha timu zao zinashiriki.
Hadi sasa bado tuna mazungumzo na baadhi ya wafadhili ila natumia nafasi hii kutoa wito na tunaomba wafadhili wajitokeze kutusaidia ili kuboresha mashindano haya.
Pia kamati ya utendaji ya TBF imesimamisha utekelezaji wa adhabu zilizotolewa na BD za kuifungia na kushusha daraja timu za Savio, Lady Lioness na Viongozi wote wa Don Bosco hadi hapo rufaa zao zitapoamuliwa hivyo wanaruhusiwa kuendelea na shughuli za michezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...