Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Elizabeth Kiondo(kushoto) akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi na vifaa mbalimbali vya maabara kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Barabara ya Mwinyi ya wilayani Temeke jijini Dar leo. Vifaa hivyo vimegharimu shilingi milioni 18. Anayepokea vitabu hivyo ni Afisa Elimu Taalum wilaya ya Temeke Rehema Mbwillo.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Elizabeth Kiondo(kushoto) akikabidhi komputya na vifaa mbalimbali vya maabara kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Barabara ya Mwinyi ya wilayani Temeke. Vifaa hivyo vimegharimu shilingi milioni 18. Anayepokea Komputya ni Afisa Elimu Taalum wilaya ya Temeke Rehema Mbwillo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Barabara ya Mwinyi akiwa katika sherehe fupi ya kupokea vitabu vya sayansi, komputya na vifaa vya maabara kutoka UNESCO. Vifaa hivyo vimetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Elizabeth Kiondo. Vifaa vyote vinathamani ya shilingi milioni 18.

Na Tiganya Vincent, MAELEZO-Dar es salaam

Tume ya Taifa ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO) imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa Shule ya Sekondari ya Barabara ya Mwinyi ya wilayani Temeke.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Profesa Elizabeth Kiondo kwa Afisa Elimu Taalum wa Wilaya ya Temeke Rehema Mbwillo.

Alisema kuwa vifaa walivyokabidhi ni vitabu vya Fizikia, Biolojia, Kemia na HIsabati vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 4 na Komputya ndogo na kubwa navyo zikiwa na thamani ya milioni 4 na vifaa mbalimbali vya maabara ambavyo vimegharimu milioni 10.

Profesa Kiondo alisema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuwajengea wanafunzi wa shule hiyo mazingira mazuri ya kujifunza masomo mbalimbali ya Sayansi kwa ajili ya kuwaanda kama wataalam wa baadaye watakaosaidia katika kuendeleza Taifa lao katika yanja mbalimbali.

Naye Afisa Elimu Taalum wilaya ya Temeke Rehema Mbwillo aliishukuru Tume ya Taifa ya UNESCo kwa kuanza kuzisaidia Shule za Sekondari za Kata kwa kuzipatia vifaa vya maabara na vitabu kwa ajili ya masomo ya sayansi.

Alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa Shule hizo ndio zinachukua vijana wengi ambao ni tegemeo la jamii na Taifa kwa ujumla katika kuchangia maendeleo na kupunguza umaskini nchnini.

Wakati huo huo Shule ya Sekondari ya Barabara ya Mwinyi ya Wilayani Temeke imechaguliwa na UNESCO kujiunga na Mtandao wa Shule zilizoungwanishwa na UNESCO duniani ya kuifanya iwe miongoni mwa Shule elfu tisa(9,000) zinazonufaika na huduma hiyo.

Akiongelea umuhimu wa mtandao huo Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Kiondo alisema kuwa mtandao umasaidia wanafunzi kujiufunza mambo mbalimbali kama vile mapambano dhidi ya UKIMWI, utunzaji wa mazingira, masuala ya jinsia.

Alisema hatua hiyo inawasaidia kutatua kutatua matatizo mbalimbali katika jamii yao na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule hiyo Isahaka Ibrahim alisema kuwa watatekeleza majukumu ya mtandao huo kwa ajili ya manufaa ya shule yao na Taifa ili ikiwezekana Shule nyingine zipate fursa ya kujifunza kutoka kwao na hatimaye wao nao waunganishwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...