Wine Emmanuel Banda akiwa katika pozi la picha na matroni wake Enes Nyuton wakati wa sherehe ya kumuaga( Send of Part) iliyofanyika katika ukumbi wa Massea Kawe jijini Dar es Salaam.
Bibi harusi mtarajiwa Wine Banda akikata keki wakati wa sherehe ya Sedd of Part yake iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Massea Kawe, kushoto ni mpambe wake Enes Nyutoni akimsaidia.
Wine Banda akiwa salon akipigwa sopsop wakati wa maandalizi ya Send of Part yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2011

    Jamani kwani ni lazima mpake make-up nyingi mpaka uzuri wenu unakuwa hauonekani? Chukueni mfano wa Kate alivyoolewa na Prince William, make-up zake zilikuwa kidogo sana ndiyo maana tuliona uzuri wake wa kuzaliwanao. Punguzeni kidogo kina dada.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2011

    Goodluck and all the best Wine(Wini?).Ndoa inahitaji uvumilivu, maisha ya ndoa ni mazuri sana yaani kama mnaelea vile au mnaogelea majini...Kuna wakati mtakutana na mawimbi makubwaaa(Hayo hayakwepeki),marefu ya kutisha huko safarini..yaani ya kutisha, lakini komaaa nayo mungu atawasaidia, ukiwa mzembe unazama..mwenzio anakuacha.Unavyocheka hapo manake umenielewa.Safi sana

    David Villa

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2011

    Tafadhali wadogo zangu, tutumie lugha vizuri iwe kiingereza au kiswahili, tusipende pinde au kubadilisha inaleta maana nyingine au kutoletaa maana hata kidogo tunavyotumia lugha kimakosa au sijui ni fesheni.

    Send Off ni tofauti na send of
    Party ni tofauti na part...

    kama vile ujasiliamali au ujasiriamali?
    kwahivyo London itakuwa Rondon au vipi?

    Ninaweza kuelewa labda kutamka kunaleta ugumu kwa mazowea za lugha zetu asili zinatuzowesha ulimi uwe hivyo, je kuandika nako vipi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2011

    MAKE-UP nyingi Wasichana na wanawake punguzeni jamani, natural beauty ni nzuri kuliko kuweka miwancha mingi namna hiyo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2011

    Wanaume mturekebishe! sisi wanawake huwa tunahisi labda wanaume wanapenda sana make ups zetu....

    Semamnachotaka tutafanya tu ili kuwaridhisha nyie.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2011

    Sasa huyo dada anaitwa Wine (mvinyo)? ama anaitwa Winnie?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 09, 2011

    Jamani hyo miwanja?Kusema ukweli ni vizuri kujiremba kiasi,na ukizingatia wao ni wasichana wadogo tu,na warembo kwanini wakakubali kuharibu picha?Namshauri siku ya harusi asijirembe hivyo tena

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...