Kikosi cha Taifa Stars.
Kikosi cha Bafana Bafana.

Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana) itachezwa Mei 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 12 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 30,000 (VIP A), sh. 20,000 (VIP B), sh. 10,000 (VIP C), sh. 7,000 (viti vya rangi ya chungwa- orange straight) na sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa (orange curve), viti vya kijani na viti vya bluu.

Bafana Bafana inatarajiwa kuwasili Mei 12 mwaka huu saa 1.30 jioni kwa ndege ya South African Airways (SAA) ikiwa na kundi la watu 30, ambapo wachezaji ni 20 wakati benchi la ufundi na viongozi litakuwa na watu 10.

Stars itaingia kambini keshokutwa (Mei 7 mwaka huu) ikiwa na kikosi kile kile kilichocheza mechi ya kirafiki Aprili 23 mwaka huu jijini Maputo dhidi ya wenyeji wao (Black Mambas).

Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...