Msanii Barnaba Elias 'Barnaba' akiimba kwa hisia katika shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda tuzo za Kili mwaka huu, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Ziara hiyo ya kuwashukuru wapenzi wa muziki waliowapigia kura imefanikishwa na wadhamini wakuu wa tuzo hiyo, Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii Joh Makini ambaye ni mmoja wa wasanii walioshinda tuzo la Kili za Muziki Tanzania 2011, akionesha umahiri wake wakati wa shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda tuzo hizo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Wasanii wateule Mwasiti Golden Mbunda 'Salasala'wakifanya vitu vyao katika shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda Kili za Muziki Tanzania 2011,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma.
Baadhi ya mashabiki wakishangilia kwa furaha wakati Msanii Joh Makini akifanya vitu vyake katika shoo hiyo.
Msanii wa The Orijino Komedi, Mpoki akiimba wimbo wa shangazi katika shoo maalumu ya ziara ya wasanii walioshinda tuzo za Kili za Muziki Tanzania 2011,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo.
PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2011

    Kaka Michuzi tupe update ya Liverpool (sorry najua hii siyo message board sahihi).

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2011

    Wapi 20% au ndo watu wanazidi kumchakachua

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...