Afisa Elimu kata ya mbezi Veroni Mallya kushoto akishuhudia Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefula (kulia)akimkabidhi Mwalimu Mkuu Zena Khakila wa Shule ya Msingi Msigani iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam, msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4.
Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimsalimu mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam mara baada ya kufika shuleni hapo kutoa msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4,anaeangalia kushoto Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Zena Khakila.
Baadhi ya wanafunzi wa shule msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, wakifurahia msaada wa madawati 50 waliyokalia yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo,shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa madawati na madarasa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, wakiangalia baadhi ya madawati kati ya 50 yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2011

    Yani hilo Dawati moja ni alfu themanini? Mbona ghali sana kwa quality hiyo...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2011

    mbona kila mahali unaandika dhamani yake au kila mmoja ajue ni sh. ngapi? anina haja kama ameamua kutoa msaada aina aja ya kujua thamani yake labda kama tungetaka kujua !!!!hiiiiiiiiiiiiiii

    Lakini ngoja nimpe sifa zake kweli vodacom mku juu wengine wanajikongoja inatakiwa waige mfano wenu hongereni sanaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...