Afisa Elimu kata ya mbezi Veroni Mallya kushoto akishuhudia Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefula (kulia)akimkabidhi Mwalimu Mkuu Zena Khakila wa Shule ya Msingi Msigani iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam, msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4.
Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimsalimu mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam mara baada ya kufika shuleni hapo kutoa msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4,anaeangalia kushoto Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Zena Khakila.
Baadhi ya wanafunzi wa shule msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, wakifurahia msaada wa madawati 50 waliyokalia yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo,shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa madawati na madarasa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, wakiangalia baadhi ya madawati kati ya 50 yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo.


Yani hilo Dawati moja ni alfu themanini? Mbona ghali sana kwa quality hiyo...
ReplyDeletembona kila mahali unaandika dhamani yake au kila mmoja ajue ni sh. ngapi? anina haja kama ameamua kutoa msaada aina aja ya kujua thamani yake labda kama tungetaka kujua !!!!hiiiiiiiiiiiiiii
ReplyDeleteLakini ngoja nimpe sifa zake kweli vodacom mku juu wengine wanajikongoja inatakiwa waige mfano wenu hongereni sanaaaaaaaaa