Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akishiriki kucheza ngoma ya Kinyatulu ya kufunda mgeni, kukundi cha ngoma hiyo kilipotumbuiza kwenye mkutano wa Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM taifa, uliofanyika katika Kijiji cha Mgori, Singida Vijijini.
Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Juma Abdallah akishangiliwa baada ya kuvishwa vazi la Kinyatulu, katika kijiji cha Mgori, Singida Vijijini. Kushoto ni Mbunge wa Iramba Mashariki, Salome Mwambu na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Singida Martha Mlata.
Msafara wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM taifa, ukikagua ujenzi wa tangi la maji la mradi wa Maji wa Mwankoko utakaohudumia Singida mjini, jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, John Chiligati akisaidia kuchimba mtaro wa mambomba kwenye mradi wa maji wa Mwankoko utakaohudumia wakazi wa Singida mjini, juzi. Wanaoshuhudia ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Juma Abdallah na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Wananchi wa Kijiji cha Nkinto, Iramba Mashariki mkoani Singida, wakimuomba Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye awape bendera za CCM, baada ya mkutano wa Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM uliofanyika juzi, katika kijiji hicho.
Wajumbea wa Sekretarieti ya NEC ya CCM na msafara wao wakipata maelezo kutoka kwa wataalam, walipotembelea chanzo cha maji cha Mradi wa Maji wa Mwankoko utakaohudumia Singida mjini,juzi. (Picha na Nkoromo Blog).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2011

    Chama cha CHADEMA chajenga N'nji,Kiitikio: Chama cha CHADEMA chajenga n'nji, CHADEMA haaaaaa, CHADEMA chajenga n;nji!

    Oh sory wajemeni, mie nilifikiri ni CHADEMA kumbe hao hapo juu ni CCM GAMBA!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2011

    bora mandamano na kusema uongo au kujitolea kusaidia miradi ya kusaidia wananchi. Tafauti ipo bwana mkitaka msitake. Operation sangara excel itawazima. You are still young CHADEMA ole wenu Nyerere kafa, angalikuwa hai mngelifyata mkia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2011

    anko umebana comment yangu... siku njema

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...