Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa Makunduchi,Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa katika ziara wilaya ya kusini na kuweka jiwe la Msingi soko katika kijiji hicho.
RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein , akifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame,baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa Tangi la Maji la,jimbo la Makunduchi, huko Kizimkazi Mkunguni jana, akiwa katika ziara wilaya ya kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Moh'd Saleh Jidawi,alipotembelea Hopitali ya Mkoa huko Makunduchi jana,alipokuwa katika ziara ya wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali na kupata matatizo ya Wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwaangalia wagonjwa katika Hospitali ya Kotej Makunduchi,akiwa katika ziara ya wilaya ya Kusini ,Mkoa wa Kusini Unguja jana.
Picha na mdau Ramadhan Othman wa Ikulu-Zanzibar
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...