Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Ualimu cha Kisanga wakiwa katika picha ya pamoja |
Chuo cha Ualimu cha Kisanga kilichopo Wazo Hill jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki iliyopita kilifanya mahafari ya kwanza tangu kuanzishwa kwa chuo hicho Agusti 5 ,2009 ambapo kilianza na mwanafunzi mmoja aitwaye Neema Lyatuu aliyesoma kwa muda wa wiki mbili bila ya kuwa na wanafunzi wengine mpaka sasa kina wanachuo 190 ambao wanachukua kozi mbalimbali ikiwemo kozi ya Ualimu ,Ualimu daraja la Tatu,na elimu ya makuzi na malezi ya Watoto (ECE) Early Childhood Development Education. Pichani juu mgeni rasmi katika mahafari hayo Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Bernard Makali akimtunuku cheti maalumu Bi. Neema Lyatuu, kwa kuwa mwanafunzi wa kwanza mwanzilishi wa Chuo cha Kisanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Kisanga Bw. Abduly Kiriwe, akiwahutubia wanafunzi hawapo pichani wakati wa Mahafari ya kwanza ya chuo hicho (kulia) Mkuu wa Chuo hicho Bw. Suleimani Kaita akiwa pembeni yake. Chuo hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2009 kina jumla ya wanafunzi 190 na mwaka huu wa kwanza wamehitimu 59.
Baadhi ya wahitimu wa stashahada ya Ualimu katika chuo cha Kisanga.
Wanakwaya wa Chuo cha Kisanga wakiimba wakati walipokuwa wakiwaaga wenzao katika Mahafali ya kwanza ya Chuo Hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...