Mdau wa Tegeta:
Kwanza, naomba huyu Mdau Mwanafunzi afafanue ni makala ipi yangu anayoijibu. Ni hii hapa ya Kiingereza:
http://www.dailynews.co.tz/ columnist/?n=12139&cat= columnist
Au hii hapa ya Kiswahili?:
http://muhunda.blogspot.com/ 2011/06/mada-yangu-ya-leo- umaskini-mbaya.html
Halafu namuomba pia ajitambulishe ni mwanafunzi wa taaluma ipi. Kwa sababu tunafahamu ni vigumu kwa mwanafunzi wa masuala ya mazingira au wanyamapori kuunga mkono ujenzi wa barabara hii. Ataajiriwa na nani?
Akishajibu, nitajaribu tena kutetea hoja zangu.
Madaraka Nyerere
Kwanza, naomba huyu Mdau Mwanafunzi afafanue ni makala ipi yangu anayoijibu. Ni hii hapa ya Kiingereza:
http://www.dailynews.co.tz/
Au hii hapa ya Kiswahili?:
http://muhunda.blogspot.com/
Halafu namuomba pia ajitambulishe ni mwanafunzi wa taaluma ipi. Kwa sababu tunafahamu ni vigumu kwa mwanafunzi wa masuala ya mazingira au wanyamapori kuunga mkono ujenzi wa barabara hii. Ataajiriwa na nani?
Akishajibu, nitajaribu tena kutetea hoja zangu.
Madaraka Nyerere
Huyo mwanafunzi anakariri tu bila kutumia akili. Nimemuuliza maswali ya msingi kabisa kuwa kama anadai barabara ikipita wanyama watamalizika kwa sababau za kelele za magari, pollution na magonjwa kutoka sehemu nyingine; mbona wanyama hao hao wanaenda kufungwa kwenye zoo mijini ambako kuna magari mengi na pollution nyingi lakini hawamaliziki? Pia nimemuuliza mbona magari ya watalii yakiingia mbugani hawasemi yataleta magonjwa na poluution? Vile vile mbona hao wanaopinga kuwepo hiyo barabara wamejenga viwanja vya ndege kwenye mbuga za wanyama katika nchi zao wakati ndege zina makelele mengi?
ReplyDeleteJambo la msingi ninalomuunga mkono ni kwamba wanyama watagongwa wengi kutokana na uzembe wa kusimamia sheria Tanzania, rushwa na usfisadi lakini si vinginevyo.
Naunga mkono ujenzi wa iyo barabara. Maendeleo duniani kote yanaleta kwa miundombinu bora ikiwemo ya barabara.Ni lazima sasa Tanzania tutetea kwa nguvu zetu mipango yetu ya maendeleo.Je wanyama ni bora kuliko watu. Mikumi national park sasa ni miongo miwili inafika kwa kupitiwa na barabara kuu ya Tunduma Dar,mbona wanyama wanaendelea na maisha yao kama kawaida.Tukiwasikiliza hawa wana-activist/and ziologist from SUA,Frankfurt Zeology society na watani wetu hatutafika. Kwa hili namkumbuka Mjomba Beni Mkapa i wish angekuwepo madarakani, barabara ingeshajengwa siku nyingi sana. Waulizeni wakazi wa Ubungo waliondamana mpaka UN kupinga ujenzi wa morogoro road maeneo ya ubungo mwisho wako wapi sasa. Kikwete waachie wakazi wa Musoma-Arusha barabara ya kuwaunganisha ili wakukumbuke siku zijazo.
ReplyDeleteWee chuchumaaa tu usilete ubishi wa kizanaki. Huyo ni mwanafuzi sasa walimu nao wakianza wewe si utaacha hata kufanya matembezi ya mshikwamano.. Huo ni ushauri wa bure
ReplyDeleteDuh Mzee umejijibu mwenyewe ataajiriwa na nani? inaonekana unajua madhara ya huo ujenzi wa barabara kwa wanyamapori kiasi ajira zinazotokana na mbuga zitatoweka..mmh yangu macho na yenu mfumbue
ReplyDeleteWewe unatumiwa kwa kuwa ni mtoto wa Mwalimu Nyerere. Lakini yetu macho. Mimi nadhani pesa tunazopata kwa utalii zina thamani kubwa kwa mfano kuliko zinazotoka kwenye migodi kwani they are not from destructive industry; na ni more sustainable kwani wanyama wanaendelea kuwepo. Sasa kama hamuoni umuhimu wa hawa wanyama, sawa lets give even permits to this so called investors wakachimbe madini humo humo serengeti kwani sisi hatujuhi kuangalia mbali. What we especially CCM are looking for is to get popularity from Mara and Arusha people so that they can be re elected. The future is not a concern of politicians
ReplyDeleteNASIKITIKA NA SIAMINI KAMA MADARAKA NYERERE HAFAHAMU KIASI HICHO ATHARI ZA KUPITISHA BARABARA SERENGETI. HIVI MADARAKA WEWE UNA WELEWA HATA KIDOGO TU WA MAMBO YA MAZINGIRA, ECOSYSTEM AMBAPO NASI TUMO, UNAFAHAMU HALI YA SASA DUNIANI IKOJE?
ReplyDeleteHIVI INA WELEWA MZURI KWELI KIASI CHA KUJILINGANISHA KAMA HAWA WANAFANYA HIVI NA SISI TUFANYE HIVI.
NAOMBA TAFUTA MTU, VITABU AU INTERNET UJIFUNZE KIDOGO TU KUHUSU MAZINGIRA. UNA FAHAMU KWAMBA SERENGETI IKO KATIKA UASILI KAMA DUNIA ILIVYOKUWA MIAKA MILIONI ILIYOPITA? UNAFAHAMU KWAMBA SASA HIVI NI SEHEMU CHACHE SANA DUNIANI ZINA HALI KAMA HIYO? UNAFAHAMU KITU KINACHITWA ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT? UNAFAHAMU KWAMBA NCHI YETU IMERIDHIA MIKATABA MBALIMBALI YA KULINDA UOTO WA ASILI, SPECIES ZINAZOPOTEA, WETLANDS NAKADHALIKA.
JINSI NINAVYOYAPENDA MAZINGIRA NATAMANI WATANZANIA WENGI ZAIDI AKIWEMO MADARAKA WAJIFUNZE KUHUSU MAZINGIRA.
NAOMBA UTAFUTE VITABU VINAVYOHUSU THREATENED HABITATS AND ECOSYSYSTEMS,FOOD CHAINS, PROTECTION AND CONSERVATIONS ESPECIALLY ZINAZOZUNGUMZIA SAVING THE EARTH'S BIODIVERSITY NAKADHALIKA.
HIVI MAWAZIRI NA WADAU WA MAZINGIRA MNALIONA SAWA HILI, SIONI KAMA MMEFANYA JUHUDI ZA KUTOSHA KUELEZA FAIDA NA HASARA ZA KUPITISHA BARABARA HII SERENGETI, HAKUNA NJIA MBADALA? WATU WAKAWA WANAWEZA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA HATA KUSAFIRI BILA KUATHIRI MAZINGIRA?
MADARAKA JARIBU KUBADILIKA NA KUJIFUNZA.
Wewe anonymous wa tano. Watanzania wote tu watoto wa Nyerere.Kama unadai Madaraka ameandika kwa kuwa ni mtoto wa Nyerere, Je, wewe ni mtoto wa nani mboba hukuweka jina lako kamili? Madaraka ni mtoto wa mkulima anatoa mawazo yake kutetea chake kama mtanzania mwingine yeyote. Usiyumbishe hoja kwa kuleta majungu na chuki. Pia ninakuomba ukiangalie kiingereza chako, ni kheri uandike kiswahili kama mimi. Michuzi maoni kama ya huyu anony wa tano jaribu kuyaepuka.
ReplyDeleteBwana Madaraka hoja ni hoja kama ni valid itapata "universal" acceptance. Huna haja ya kujua huyo aliekujibu anasoma fani gani. Wanaofanya maamuzi kwa masuala kama haya wanapima hoja za aina tofauti si lazima za fani moja tu. Vile vile kwa mtu kama mimi niliesoma hoja zako na zake, hoja zake mwanafunzi zimeni convince zaidi kuliko zako. Tunapojadiliana mambo mbali mbali kwenye blogu si lazima tuanze kusema fani zetu, tunaelimishana kwa hoja tu. Si ajabu akijibu sasa kukuambia fani yake utamuuliza amesoma kiwango gani? nchi gani? ana uzoefu wake, kabila lake, umri wake, nk. Haya hayana maana as long as mtu anatoa hoja nzito zinazoeleweka. Salam zao Musoma.
ReplyDeleteserengeti kubwa sana bana, kwani Mikumi hakuna wanyama? si road imecross mbugani? Tujenge network tuache na siasa za mazingira. Tz bado pori kubwa sana anywhere sory nimechangia kilayman lakini habari ndo hiyo
ReplyDelete